22.11.13

Friday, June 14, 2013

(News) CHAMA CHA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA (TUMA)

CHAMA CHA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA TANZANIA (TUMA)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI   14-6-2013
Chama cha muziki wa kizazi kipya Tanzania (TUMA) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa msanii mahiri wa Hip Hop nchini marehemu Langa Kileo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari,marehemu Langa Kileo alifariki siku ya jana jioni katikia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipopelekwa kwa ajili ya matibabu.
Tasnia ya muziki nchini imepata pigo lingine tena kwani ni takribani muda wa wiki 2 tokea msanii mwingine mahiri Albert Mangweha afariki Dunia akiwa nchini Afrika Kusini na kuzikwa  katika makaburi ya Kihonda yaliyopo Mkoani Morogoro.
Tunapenda kutoa wito kwa wasanii wote nchini kujitokeza kwa wingi na kuonyesha upendo pamoja na kutoa ushirikiano katika kipindi hiki kugumu cha msiba wa msanii mwenzetu Langa Kileo.
Chama kinatoa pole kwa familia ya marehemu,ndugu,jamaa,marafiki na mashabiki wote wa muziki nchini na kuahidi kutoa ushirikiano katika wakati huu mgumu kwetu sote.
Tunaamini tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi,Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Langa Kileo.
Amin.
Fredrick Gerson Mariki
Mwenyekiti wa TUMA (TANZANIA URBAN MUSIC ASSOCIATION)

No comments: