22.11.13

Wednesday, June 12, 2013

(News) Orijino Komedi wasaini mkataba mpya wa usimamizi

Kundi la kipaji cha televisheni “Orijino Komedi” linaloongoza nchini kwa vipindi vyake kupitia television imeingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa kushirikiana na Rockstar 4000. Mkataba huu unakuwa wa kwanza kwa wasanii wa luninga kupitia kampuni ya Nexus.


Nexus imenunua haki zote za usimamizi wa biashara na uongozi wa kundi hilo ambalo linajulikana sana nchini kupitia vichekesho vyake kupitia vituo vya televisheni na matamasha mbali mbali ambapo mkataba huu utakuwa ni kwa ajili ya kusimamia kipindi hiki cha vichekesho kinachoundwa na wachekeshaji saba wajulikanao kama; Joti, Maclegan, Masanja, Wakuvanga, Mpoki, Vengu na David Seki ambacho kimekuwepo hewani kwa mfululizo wa miaka sita.
Kushirikiana na Orijino Komedi ni kitu cha muhimu kwa Nexus kwani siku zote imekuwa ikitamani kufanya kazi kwa karibu na kundi hilo na kuthamini kazi zao kutokana na vipaji vya hali ya juu walivyokuwa wakionyesha wasanii wa kundi hilo; alisema Mkurugenzi mkuu wa Nexus, Bwana Bobby Bharwani.
“Nimefurahishwa sana kufanya kazi na watu wenye vipaji vya hali ya juu na kuiingia mkataba na Kampuni ya Nexus Agency. Kwa pamoja tumedhamiria kukuza na kubadilisha dhama ya vipaji na sanaa kutoka ilipo na kuwa ya kimataifa” alisema Christine “Seven” Mosha , Mkuu wa kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara kutoka ROCKSTAR4000.
Muandaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni Davis ‘Seki’ amesema wanafuraha kuingia mkataba wa kazi na kampuni ya Nexus Agency na Rockstar 4000 Africa, ambapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kukidhi haja ya soko.
Kwa kushirikiana na Rockstar 4000, nexus inatambua na kuthamini vipaji hivyo itahakikisha inaendeleza vipaji vya wasanii wa kundi hilo ili vipaji vyao viweze kufikia kiwango cha juu vya ufanisi ndani ya Afrika na kimataifa kwa ujumla.
Jiunge na kufuatilie Orijino Komedi mtandaoni kupitia;
Tovuti
www.orijinokomedi.com

YouTube
www.youtube.com/orijinokomedi

Twitter
www.twitter.com/orijinokomedi

Facebook
www.facebook.com/orijinokomedigroup

Mwisho
NEXUS CONSULTANCY AGENCY
Bobby Bharwani
CEO

ROCKSTAR 4000
Christine ‘Seven’ Mosha
Head of Talent and New Business

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Tabasamu PR Consultancy
lucy@tabasamupr.co.tz
+255 754 602 674  
                     

No comments: