Vodacom Tanzania Head of Key Accounts and Franchise, Upendo Richard
(right) hands over keys to Miriam Minja, the Manager of Vodacom Shop at
Millennium Towers, Dar es Salaam, during the official opening of the
shop. Looking on is Vodacom Tanzania Head of Corporate Communications,
Joseline Kamuhanda.
Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom
Tanzania, Bi.Upendo Richard(kulia)akimkabidhi funguo Meneja wa duka
jipya la Vodacom lililopo Millennium Tower ghorofa ya kwanza Bi.Miriam
Minja,ikiwa ni inshara ya uzinduzi rasmi wa duka hilo.Anaeshuhudia ni
Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi.Joseline
Kamuhanda.
Meneja wa duka jipya la Vodacom lililopo Millennium Tower ghorofa ya
kwanza Bi.Miriam Minja,akifungua duka hilo kwa mara ya kwanza tayari kwa
kutoa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo,akishuhudiwa na Mkuu wa Idara
ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania, Bi.Upendo Richard(kulia)na Mkuu
wa kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano wa kampuni hiyo
Bi.Joseline Kamuhanda.
Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania Bi.Joseline Kamuhanda,akiongea na waandishi wa habari wakati wa
uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo lililopo Millennium Tower
ghorofa ya kwanza.Tayari kabisa kwa kutoa huduma kwa wateja wake.
Miriam
Minja (right) the Manager of Vodacom Shop at Millennium Towers, Dar es
Salaam, shows the features of a phone to Lameck Hanold, a customer who
visited the shop during its official opening. Looking on on the left is
Vodacom Tanzania Head of Key Accounts and Franchise, Upendo Richard.
• Watanzania zaidi kuendelea kupata huduma za mawasiliano.
Dar
Es Salaam, June 18, 2013 … Huku jiji la Dar es Salaam likiendelea kukua
kwa kasi na kushuhudia ongezeko kubwa la watu kutoka sehemu mbalimbali,
upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii umekuwa ukikabiliwa na
changamoto kadhaa kutokana na kasi ya utoaji huduma kutoendana na kasi
ya ongezeko la watu.
Katika kukidhi haja hiyo ya utoaji wa huduma kwa
wateja na elimu kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeendelea kupanua wigo wa ajira na
huduma kwa kufungua duka la huduma kwa wateja katika jengo la Milenium
Tower lililoko Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia wakati
wa uzinduzi wa duka hilo, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa
Vodacom Tanzania Joseline Kamuhanda, amesema Vodacom ni kampuni pekee
ambayo imeendelea kuongoza kwa kuwa na maduka mengi ya mauzo na huduma
kwa wateja kwa kufikisha maduka 66 ikiwa ni kampuni pekee kuwa na maduka
mengi ya huduma na kufanikisha adhma ya kukidhi mahitaji ya huduma kwa
wateja wa kampuni hiyo, huku Dar es Salaam ikiwa na idadi ya maduka 21.
“Ukuaji
wa huduma kwa kampuni ya Vodacom umekuwa kwa kasi, huduma kama ya M –
Pesa sasa imepanuka kwa kasi na kutoa huduma kwa watanzania zaidi ya
milioni 10. Kufuatia mafaanikio haya tunalazimika kuhakikisha
upatikanaji wa huduma kwa wateja ni wa uhakika” alisema Kamuhanda na
kuongeza kuwa,
“Kuongoza katika sekta ya mawasilaino kuna changamoto
zake, lazima tuhakikishe tunaendana na kasi ya ukuaji na ongezeko la
watu na uhitaji wa huduma zetu kwa watu wa aina mbalimbali.
Aidha
Kamuhanda alisema kuwa Kufunguliwa kwa duka hilo sasa sio tu kunaboresha
upatikanaji wa huduma pia ni fursa pekee ya kuendelea kupanua wigo wa
ajira kwa watanzania.
“Ufunguzi wa duka hili unatoa fursa ya ajira
kwa watanzania, ambapo wafanyakazi wapatao 3 watatoa huduma kwa wateja
wetu hivyo ni hatua kubwa kwa kutengeneza ajira kwa wafanyakazi wapya.
Hadi kufikia sasa, Vodacom imetoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi
500 na wengine zaidi ya 450,000 wenye ajira zisizo rasmi,” alisema
Kamuhanda.
Mwisho…….
No comments:
Post a Comment