22.11.13

Wednesday, June 26, 2013

(News) WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU RUVUMA WATOA WITO

 Meneja wa Mradi wa MWEI wa Vodacom Tanzania,Bi.Mwamvua Mlangwa(kushoto)akimkabidhi moja ya msaada mhasibu wa kituo cha watoto yatima cha Ujirani mwema kilichopo Songea mkoani Ruvuma.

 Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa na Michael Kipuyo wakiwa katika picha ya pamoja na watoto waishio kwenye mazingira hatarishi wa kituo cha Ujirani Mwema wilayani Songea baada ya kukabidhi msaada wa chakula na vifaa mbali mbali kwa watoto zaidi ya 60 wanaolelewa hapo.

Meneja wa Mradi wa MWEI wa Vodacom Tanzania,Bi.Mwamvua Mlangwa(kushoto)akimfariji mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ujirani mwema kilichopo Songea mkoani Ruvum,Mara walipotembelea kituo hicho kwa lengo la kutoa misaada mbalimbali. 

Watoto waishio kwenye mazingira magumu wa Mkoani Ruvuma,wametoa wito kwa makampuni na jamii kwa ujumla kutowasahau katika kuwalea na kuwatembelea mara kwa mara siyo kusubiri wakati wa sikukuu tu.Waliyasema hayo katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika 2013 mara walipotembelewa na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wa mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na timu ya MWEI iliyofika mkoani humo kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa wakinamama.
Watoto hao waliomba wadau kuiga mfano wa Vodacom Tanzania kwani hiyo itakuwa changamoto kwao kuweza kutimiza yale yanayotegemewa kutoka kwao na hatimae kuwa Watanzania wenye ari ya kuleta maendeleo na mafanikio chanya katika taifa.
Wafanyakazi hao walifika hapo kwa lengo la kuwaona na kuwafariji pia na kutoa msaada wa kilo 100 za mahindi, sabuni na mafuta ya kujipaka pamoja na viburudisho mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho chenye watoto 64.
Akizungumza kwenye makabidhiano ya msaada hiyo, Meneja wa Vodacom Ruvuma Bw. Michael Kipuyo alisema kuwa wameona ni kipindi kizuri kuwakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwasaidia nao wajisikie ni sehemu ya jamii inawajali.
"Vodacom tunajali wateja wetu wa sasa na wale wa baadae kwani kwa kusaidia watoto hawa tunasaidia jamii na serikali kulea watoto ambao watakuja kuwa ni nguvu kazi ya taifa hapo baadae katika mazingira ya amani na hatimae kuwafanya wajisikie kuwa ni sehemu ya jamii." Alisema Kipuyo.
Watoto hao waliwashukuru wafanyakazi hao wa kampuni hiyo kwa kuwakumbuka katika kipindi hiki Afrika inapoadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika na kuwakumbuka wale waliofariki katika kudai haki zao kule Afrika ya Kusini mwaka 1976.
Watoto hao walitoa wito kwa makampuni na jamii kwa ujumla kutowasahau katika kuwalea na kuwatembelea mara kwa mara siyo kusubiri wakati wa sikukuu tu.Waliomba wadau kuiga mfano wa Vodacom Tanzania kwani hiyo itakuwa changamoto kwao kuweza kutimiza yale yanayotegemewa kutoka kwao na hatimae kuwa Watanzania wenye ari ya kuleta maendeleo na mafanikio chanya katika taifa.
Mwisho.

No comments: