22.11.13

Thursday, July 25, 2013

(News) Hali ya Msanii nguli wa maigizo hapa nchini Tanzania, Ndg Said Bin Wangamba almaarufu kama Mzee Small inaendelea vizuri

 
Taarifa / Mrejesho : Hali ya Msanii nguli wa maigizo hapa nchini Tanzania, Ndg Said Bin Wangamba almaarufu kama Mzee Small inaendelea vizuri, na ANASHUKURU sana kwa wale wote wanaomkumbuka katika kipindi hiki kigumu cha maradhi. Kwa sasa anaweza kujikongoja taratibu mwenyewe., 

Anaendelea na mazoezi ya kila siku, na kubwa ni dozi ya dawa kwa ajili ya kumsaidia kuondoa uvimbe uliogundulika miezi kadhaa iliyopita, kichwani mwake ambapo dozi moja tu inagharimu takribani 30,000TZS pamoja na mahitaji mengine ya lazima ya kila siku,
 Kwa yeyote atakaeguswa tafadhali unaweza kuwasiliana na Mzee wetu kupitia, M-PESA kwa kutumia namba ya Said Ngamba (Mzee Small) 0754647265 na TIGO PESA kwa kutumia namba ya mkewe 0658111311,

Changamoto: Ni Wakati MUAFAKA Sanaa kuwa Ajira Rasmi na yenye MAPATO STAHIKI,

Alituchekesha na kutuondolea uchovu kwa kipaji chake, nasi tumkumbuke na kumuenzi,
Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M Chuma

No comments: