Mratibu
wa Tamasha la RAHA ZA JANA NA LEO Bw.Kahabi Ng'wendesha akilitambulisha
rasmi Tamasha hilo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar katika hoteli
ya Chichi iliyopo manispaa ya kinondoni jijini Dar.
Bw. Kahabi alizungumzia namna kampuni ya Yuneda namna
ilivyojiandaa kufanikisha tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na wakazi
wa jiji la Dar jumamosi hii katika viwanja vya posta kijitonyama.
Baadhi
ya viongozi wa bendi tofauti wakiwa katika mkutano na waandishi wa
habari kuthibitisha ni namna gani wamejiandaa naTamasha hilo
linalokutanisha bendi sita za muziki wa dansi nchini Tanzania.Bendi hizo
ni Mashujaa,Bantu group,Twanga pepeta,Msondo,Sikinde na king
kikii"wazee sugu".
Mwanamuziki
Bichuka(Sikinde) akifafanua namna watakavyoiburuza Msondo Ngoma
jukwaani ikiwa ndiyo waasimu wao wa siku nyingi kwa mara nyingine
wanakutana jukwaa moja viwanja vya posta.Pia kutakuwa na silent moment kuwakumbuka wanamuziki wote wa mziki wa dansi waliotangulia mbele ya haki nchini Tanzania.
King
Kikii(kushoto) akielezea namna alivyojipanga kuteka mashabiki siku ya
jumamosi hii katika viwanja vya posta .kulia ni mwanamuziki mkongwe
Hamza Kalala.Milango ya uwanja itakuwa wazi kuanzia saa tano asubuhi
hadi usiku mnene,Watoto bureeee mpaka saa kumi na mbili,wakubwa Tsh
8,000/= tu mpaka chwee.Michezo ya watoto,nyama choma na vinywaji
vyakutosha vitakuepo.
No comments:
Post a Comment