Msanii Rukkii anayejulikana
kama Sweetty Rukiah Mohamed au Rukiah Mohamed ameangusha bonge la ngoma
inayoitwa ‘Mimi na Wewe’ featuring Christian Bella.
Akiongea baada ya kuachia
hii ngoma, Christian Bella alisema alifurahi sana kufanya huu wimbo na yuko na
uhakika ni wa hali ya kimataifa. Ngoma hii imefanyika chini ya producer KGT
kutoka studio za G-Records.
Rukkii alionekana kwa mara
ya kwanza kwenye runinga katika tamthilia ya ‘Mtazamo’ ambayo ilikuwa inarushwa
hewani kwenye kituo cha televisheni cha Channel TEN.
Mwaka wa 2012 ulikuwa mwaka
mzuri kwa Rukkii, alishiriki katika shindano la ‘Imba Cheza Vaa kama Rihanna’
liloandanliwa na Global Publishers/Dar Live akishindania shilingi millioni
kumi. Baadaye, alicheza filamu ya ‘Thecla’ na ‘Lugha Mseto’ zilizozambaswa na
kampuni ya Whatever Films Production na Pili pili Entertainment. Lugha Mseto ni
movie ambayo umempa umaarufu sana nchini. Hii filamu inaonyeshwa kwenye mabasi
ya mikoani na pia kipande chake kimesambaa Whatsapp.
Mapema 2013, Rukkii alikuwa
signed chini ya music label ya FMA - Flave Music Afrika.
‘Nimefurahi sana kupata
sehemu ya kukuza kipaji changu cha mziki na kutimiza ndoto zangu za kuwa msanii
wa kike bora Tanzania, Afrika mashariki na Africa nzima kwa ujumla’ Rukkii
amesema.
Twitter @sweettyrukkii Facebook page - Sweetty Rukiah - Rukkii
Thanks for your support.
No comments:
Post a Comment