22.11.13

Tuesday, September 03, 2013

(News) M-PESA SASA RASMI KUKUSANYA ADA YA LESENI YA MAGARI

 Meneja Uhasibu wa Maxcom Africa,Bi.Lucy Kanza akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Road License kwa kutumia huduma ya M-PESA.Wanaoshuhudia katika ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo.


 Mmoja wa waandishi wa habari  kutoka kituo cha Channel Ten Bw.Fred Mwanjala(katikati)akiuliza swali katika uzinduzi wa mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Raod License kwa kutumia huduma ya M-PESA.

 Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa (katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Raod License kwa kutumia huduma ya M-PESA.Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo na kushoto ni Meneja wa Uhasibu wa Maxcom Africa,Bi.Lucy Kanza. 

 Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)wakifuatilia jambo kwa umakiini wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Raod License kwa kutumia huduma ya M-PESA.

Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini - TRA leo imezindua rasmi mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Raod License kwa kutumia utatartibu wa M-pesa huku tayari mfumo huo ukionekana kukubalika zaidi na walipa kodi hiyo nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es salaam Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa kampuni ya Vodacom Kelvin Twissa amesema kuzinduliwa kwa utaratibu huo ni mwendelezo wa namna ambavyo maisha ya watanzania yanavyozidi kuwezeshwa kuwa rahisi wakati ambapo M-pesa inazidi kuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ya Mtanzania.
Twissa amesema ukuaji wa kasi wa matumizi ya M-pesa unathibitisha umuhimu wake hapa nchini na kuongeza kuwa kutumika kwenye ukusanyaji wa kodi ni hatua nyingine muhimu kwa faida ya walipa kodi ambapo sasa M-Pesa ni sehemu ya maisha ya watanzania na hakuna tena sababu ya kupanga foleni ndefu na kutumia muda mwingi.
"Ni Wakati mwingine M-pesa inavyowapa wananchi na walipa kodi wengine wote hapa nchini utataribu mwepesi, rahisi, salama na wa uhakika zaidi wa kulipa ada  za leseni ya magari kwa urahisi zaidi wakati wowote mahali popote."Alisema Twissa 
"Tunapotambua umuhimu wa kodi kwa maendeleo ya nchi hatuna budi kufurahia hatua hii ambayo tayari katika kipindi cha muda mfupi kisichozidi wiki mbili M-pesa imeshaonesha mafanikio makubwa katika makusanyo, hili linatupa furaha kama kampuni na ni wazi kila mmoja analifurahia."Aliongeza Twissa
Twissa amesema Vodacom itaendelea kuuwezesha mfumo wa M-pesa kuwa wenye kutoa suluhisho la masuala mengi zaidi ili kukidhi shabaha ya kampuni hiyo ya kubadili maisha ya watu kupitia teknolojia ya huduma za simu za mkononi.
"Tumekuwa imara wakati wote tangu M-pesa ilipozinduliwa nchini mwaka 2007, hata hivyo bado tunashauku ya kufanya mapinduzi makubwa zaidi kupitia M-pesa tukitambua kwamba hiyo ni kiu ya kila mmoja kuzingatia kile ambacho tayari M-pesa inayaywezesha kupitia viganja vya mikono yao."Alisema Twissa
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo amesema M-pesa imeleta urahisi zaidi kwa Mamlaka katika ukusanyaji wa ada za leseni ya magari .
"Ni jambo jema kwa mamlaka kuona inawapatia wateja wake(walipa kodi)utaratibu rahisi zaidi kwao katika kuwawezesha kutimiza wajibu wao wa kisheria wa kulipa kodi pasi na kuwepo usumbufu wa aina yoyote huku pia utaratibu huo ukileta ufanisi kwa mamlaka."Alisema Kayombo
Amesema TRA ina imani kuwa ushirikiano wake na Vodacom utakuwa wenye tija zaidi katika siku zijazo kwa kuhakikisha mfumo wa M-pesa unatoa uwezo zaidi kwa walipa kodi kuutumia katika kuleta urahisi kwao kulipa kodi mbalimbali.
Inakidiwa kuwa katika kipindi cha wiki mbili TRA imekusanya kaisi cha Bilioni 2 cha malipo ya ada za magari kupitia M-pesa pekee.
Mwisho.  

No comments: