22.11.13

Monday, September 23, 2013

(News) Mamia wajitokeza Usahili wa Vodacom Zanzibar Fashion Week

 Baadhi ya wanamitindo waliofuzu katika awamu ya kwanza ya usaili wa wanamitindo watakaoshiriki maonesho ya Vodacom Zanzibar Fashion Week wakiwa katika picha ya pamoja na majaji pamoja na waandaaji wa Maonesho hayo yatakayofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 27 Visiwani Zanzibar Mara baada ya kumalizika kwa usaili uliofanyika katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mchujo mwingine utafanyika visiwani Zanzibar mwisho wa wiki hii.
 Baadhi ya wanamitindo waliojitokeza katika usaili wa wanamitindo watakaoshiriki katik amaonesho ya Vodacom Zanzibar Fashion Week wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa usaili huo uliofanyika katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Maonesho hayo yatakayofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 27 Visiwani Zanzibar. Mchujo mwingine utafanyika visiwani Zanzibar mwisho wa wiki hii.

 Washindi wa mchujo wa mwisho wa Maonesho ya mitindo ya Vodacom Zanzibar Fashion Week yatakayofanyika visiwani Zanzibar kuanzia tarehe 25 hadi 27 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa washindi. Zaidi ya wanamitindo 100 walihudhuria usaili huo uliofanyika katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na wanamitindo 10 kuibuka kidedea. Mchujo mwingine utafanyika visiwani Zanzibar mwisho wa wiki hii.

 Muandaaji na Mkufunzi wa masuala ya mitindo Farokh Abdallah akitoa mafunzo kwa wanamitindo waliojitokeza kufanya usaili wa kushiriki katika Maonesho ya Vodacom Zanzibar Fashion Week yatakayofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 27 visiwani Zanzibar Usaili huo ulifanyika katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mchujo mwingine utafanyika visiwani Zanzibar mwisho wa wiki hii.

No comments: