22.11.13

Saturday, October 19, 2013

Mashairi ya "MDUDU" kutoka kwa SOLO THANG akiwa na MR. BLUE

MDUDU ni nyimbo mpya ya SOLO THANG inayotarajiwa kutoka hivi karibuni akimshirikisha MR BLUE  kwenye kiitikio!! MDUDU ni nyimbo ya kwanza kutoka katika album inayofata ya Solo Thang,ambayo itajulikana kwa jina S.U.M.U (Sitaki Ujinga Maradhi na Umaskini)

MSANII:  SOLO THANG ft MR BLUE
JINA LA NYIMBO:  MDUDU
STUDIO: CLOUD 9 (BELFAST), DEFATALITY (DSM)
PRODUCERS: SNIPER G GANJI (BEAT),MESSEN (MIXIN & MASTERING)
AUTHOR: SOLO THANG

iNTro
(DEFA
TALITY MUSIC)
YOU KNOW WHAT TIME IT IS   
ITS YA BOY BACK          (HELLO HELLO HALOOOO)
SOLO THANG                  (ULAMAA)
AAAAAH THIS TIME AROUND
I THINK WE NEED "DUDU KILLER"  (LETS GO NOW)

VERSE 1:
EYO NAKUPA MFANO NJAA ,NA HUYU MDUDU WANAFANANA
SI UNAKULA KILA SIKU ,ILA NJAA INARUDI TENA
MDUDU ANACHEZA NA FEELINGS DAWA KAIIMBA MARVIN GAYE

(SEXUAL HEALING?) , HAUPONI MDUDU YUPO EVERY DAY
SIO KUNGUNI ILA ,NAE ANAPENDA KITANDA
NDIO LOCATION KAMA MOVIE, ACTION- KUNG FU PANDA
YE ANAPENDA NJIA PANDA KAMA UMBO LA MANATI
NDANI YA FIKRA KAKUJAZA KUWA, NISHATI  MIHADHARATI
SIO FUNDI BILA SPANA NA, ANALEGEZA MACHO
HAKITOSHI ULICHONACHO SHARTI UPATE CHA MWENZAKO

YE NDIO CHANZO CHA MAYAI ALIPOMVA KUKU
NDIO KISA JOGOO HUWIKA WEWEEE MAMBO IPO HUKU 
HAICHEKESHI WE UNACHEKA, NDIO UJUE TAYARI
HAKUNYESHI WE UMELOA USIJISHIKE TAFADHALI
NA SIO SHETANI USEME ANAPANDA KWA UBANI 
NA SIO WA KOKWA LA EMBE NAMBIE NI MDUDU GANI??


CHORUS
CHEKI MDUDU ANAVYOWASHAAAAA (washa washa)
ANANIFANYA NINAKUA BWEGE
AKILI ZINAKUA NA MATEGE
ANACHOTAKA NDIO NAFANYA ANACHOTAKA NDIO NAFANYA!!

VERSE 2
SI BORA ANGEKUA PANYA UWEKE SUMU AMA MTEGO
PALE PALE KWENYE SHIMO HAHAAAA NDAGA FIJO
WATU NATEMBEA NA "PUMP" KAMA MAFUNDI BAISKELI
KAZI KUJAZA WATU UPEPO NA "BLADDER' ZINAJAA KWELI

HANA SINDANO SIO DONDORA USEME MPIRA KAUTOBOA
BILA ZANA USICHEZE RAFU, REFA KADI ASIPOTOA?
WE HAMIRA YE NI NGANO LAZIMA MMOJA ANAVIMBA 
OGOPA SANA HUYU MDUDU ANATISHA KAMA SIMBA

KANGA MOJA NDEMBE NDEMBE ETI LAKI SI PESA
NA HAUWEZI KUISHI KAMA BURUDA BROTHER KAKA UTAJITESA
ILA MDUDU AKIKUPA NGOMA NENDA KANUNUE GUITAR
NDIO SAFARI UNAENDA ANZISHA BENDI KAKA FUTI SITA

SIO MBU USEME UTAPATA MALARIA 
YE ANASAMBAZA UGONJWA AMBAO UNAITWA SEX-ERIA
NA SIO SHETANI USEME ANAPANDA KWA UBANI 
NA SIO WA KOKWA LA EMBE NAMBIE NI MDUDU GANI??

CHORUS
CHEKI MDUDU ANAVYOWASHAAAAA (washa washa)
ANANIFANYA NINAKUA BWEGE
AKILI ZINAKUA NA MATEGE
ANACHOTAKA NDIO NAFANYA ANACHOTAKA NDIO NAFANYA!!

VERSE 3

UKIBANWA NA KIKOHOZI, NI LAZIMA UKOHOE
VIPI UKIBANWA NA MDUDU JIBU NENDA KAKOKOTOE
JAMAA KASHIKIWA PANGA AKAAMBIWA LAMBA MCHANGA
AKAGOMA AKATOKA NDUKI BREKI YA KWANZA KWAO UPANGA
JOLY, KAMKUTA DEMU, YULE DEMU AKAONYESHA SHANGA
HADHARA NDIO IKAWA CHUMBA!, MAANA MDUDU KASHAPANDA

SIO KWAMBA ALIKUA NA NJAA, ILA 'SHAWTY" KALA KONI
SI ANA KIU? MPE MAJI SASA BROTHER KULIKONI??
YEAH SIJAPATA KUONA MKATE MGUMU MBELE YA SUPU
VIPI NGOZI ZA UDONGO MZIGANDISHE KAMA SUMAKU?

INGAWA UMBO SIO CHAKULA, WATU UDENDA UNAWATOKA
UTASKIA KASHATAFUNWA, JIULIZE MWILI BANZOKA?
HUU MCHEZO USIO NA DRAW, LAZIMA MTU APIGWE BAO
UCHU KAMA MPENDA NYAMA, HAWA WADUDU NDIO ZAO
NA SIO SHETANI USEME ANAPANDA KWA UBANI 
NA SIO WA KOKWA LA EMBE NAMBIE NI MDUDU GANI?


CHORUS!
CHEKI MDUDU ANAVYOWASHAAAAA (washa washa)
ANANIFANYA NINAKUA BWEGE
AKILI ZINAKUA NA MATEGE
ANACHOTAKA NDIO NAFANYA ANACHOTAKA NDIO NAFANYA!!


fOLLOW US ON TWITTER
@TeamSOLOThang
@SoloThang

TEMBELEA HAPA ILI UWE WA KWANZA KUISIKIA "MDUDU",,,STAY TUNED!!!!

No comments: