Friday, November 22, 2013

NAWASHUKURU SANA KWA KUTEMBELEA DJCHOKAblog SINCE 2009

Mambo vipi wadau...
Imekuwa ni muda mrefu sana tumekuwa wote tokea 2009 mpaka leo hii na bila kutetereka, nimepita vishawishi vingi mabonde na milima na vyote nikavivuka huku nikiwa na nyinyi wadau wangu wa DJCHOKAblog. 

Nilishakatishwa tamaa lakini nikamweka mungu mbele na nikasema nitavishinda vita hivi, na leo najaribu kusema naendelea kumwomba mungu huu mziki ninaupiganie ufike sehemu hata usipofika lakini naweza subutu kusema nilijaribu kidogo. 

Natoka rasmi kwenye blog nahamii kwenye website, nilikuwa namajina mengi sana yakuiita hii website yangu mpya lakini majina hayo yote yangu yameshawahiwa na watu nisiowajua na wakanunua Domain na kuzimiliki. Lakini sikukata tamaa ndipo nikaona niite website hii yetu kwa jina la DJ CHOKA MUSIC. Nikiwa na maana vitu vitakavyokuwa ndani ya hii website asilimia 90 ni mziki na habari za wasanii wetu wa nyumbani. Bado sijajua mbele kukoje ila naomba ushirikiano wetu ili tuweze kuuvuka huu mto mkubwa ambao uko mbele yetu.

SINA CHA KUWALIPA ZAIDI YA ASANTE KWA KUTEMBELEA DJCHOKAblog NA ASANTE KWA WEWE MDAU WANGU MZURI UNAYENIOMBEA MAZURI KILA KUKICHA NA ASANTE WEWE ADUI YANGU UNAEPENDA KUKATISHA MAENDELEO YANGU.

NAWEZA KUSEMA MANENO HAYA MACHACHE TU
Maisha ni kuendelea hadi zamu yangu ya kushinda ifike. Sikatishwi tamaa na kushindwa ndipo nitaona kuwa ugumu nikipindi cha mapito kuelekea mafanikio.
 
NAWAPENDA SANA

It's me
DJ CHOKA aka MR APPETITE

No comments:

Post a Comment