22.11.13

Monday, November 09, 2009

WAKALI WA ZOUK TANZANIA MPO TAYARI?

Msanii mpya wa mahadhi ya ZOUKanayekuja juu kwa kasi ya ajabu zaidi ya kimbunga cha TSUNAMI,ni zao jipya kutoka Nyanda Za Juu Kusini nazungumzia wilaya ya Njombe ndani ya mkoa wa IRINGA ni msanii anayejulikana kwa jina la kisanii AMANIWETU jina lake halisi ni AMANI SAID KILLO,anaingia kwenye ulingo waZouk akijitambulisha na wimbo wake mpya uitwao 'MAPENZI NI ZAWADI'ikiwa ndio maandalizi ya Album yake ya kwanza itakayo kwenda kwa jinala MOYO FICHO LA SIRI.mpaka sasa amesharekodi nyimbo nne katika studioya SOUND POWER chini ya Producer B jayzee(THE PROVIDER) studio hiyoipo Njombe mjini.Mpaka sasa kazi ambazo amesharekodi ni pamoja na MAPENZI NI ZAWADI,RAFIKI,MOYO FICHO LA SIRI na WAUZA SURA na kazinyingine mpya inayopikwa jikoni kwa sasa inaitwa NIMEMPATA,Hivyoanaomba wapenzi wa muziki wa Zouk wakae tayari kwani mwanzoni mwamwaka 2010 album yake itakuwa sokoni

No comments: