22.11.13

Thursday, November 26, 2009

ZIARA YA FID Q MJINI BAGAMOYO (KAOLE).

Huu mti unaitwa Mbuyu una miaka mingi sana tena umeshavuka karne.

Aliyekaa katikati ni Makamua msanii wa bongo fleva ambaye kwa sasa yuko Bagamoyo anakula kitabu kidogo, tulimkuta huku na tukamuomba tuwe nae katika kujifunza mambo mawili matatu, hapa tulikuwa tunapewa somo kabla yakuanza kutembea.

Shabiki wa Fid Q akiwa na bwana farid

Kama unavyojionea makaburi ya viongozi wa zamani, hapa tuliambiwa kaburi lenye mnara mrefu kuliko wenzake basi huyo alikuwa kiongozi mkubwa sana kwa wakati huo.

Michael wa Babkubwa akiwa na Edmond Azaza, hawa nao tulikuwa nao katika safari yetu.

Hapa alipokaa dj choka ni Kaburi la mke na mume (Wapendanao), kaburi hili wamezikwa mume na mke waliokufa siku moja kwa ajali katika bahari ya Hindi na kuzikwa kwa Pamoja.

Fid Q akiwa kwenye pozi la kihistoria nyuma yake ndio hayo makaburi ya watu wazamani.

Hapa washkaji walikuwa kwenye kisima ambacho hakijawahi kukauka maji na wanasema maji hayo huwa yapo hivyo hivyo hata huyapunguze vipi, washkaji wakinawa kwa pamoja.

Fid Q akichota na yeye hayo maji na kuanza kunawa, picha hii walikuwa wakinawa na Michael aka M X

Timu nzima iliyomsindikiza Fid Q ikiwa kwenye pozi la pamoja.

Baadae tuliingia kwenye gereza ambalo mababu zetu walikuwa humo, hapa fid akiwa anaionyesha picha ya ABUSHIRI, huyu alikuwa mfanyabiashara mashuhuri katika eneo la mwambao mwa afrika ya mashariki kuanzia Bagamoyo hadi Tanga.

Hapa ni nje ya gereza hilo kama unavyojionea sanamu la mfungwa akiwa amebeba pembe ya ndovu.

Unabishaaaaaaaaaaaa... baada ya kuzunguka kote tukapitia msosi kidogo, mimi hapa ndio nashiba. Kaa humo

3 comments:

Anonymous said...

C MCHEZO UO MLO

Mzee wa Changamoto said...

Hii ni kati ya post njema saana kuwahi kuisoma hapa. Ni SANAA NA JAMII. Ni VIJANA WAKISAKA HISTORIA MUHIMU KWAO na ni WATOTO WA MJINI WAKITEMBELEA VIJIJI VILIVYOWEKA HISTORIA,
Big up kwa Fid Q na waandaaji wa ziara, kwa washiriki ote wna KWAKO Choka kutuonesha hili.
Blessings

Anonymous said...

mama yanguuuuuuuuuuuuuuuuuuu


its mirinda