22.11.13

Tuesday, December 08, 2009

LEO NDIO LEO NJOO UBURUDIKE NA MSONDO NGOMA.

BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini Msondo Music bandi leo watafanya utambulisho wa albam yao mpya ya huna shukrani kwa sataili ambayo aijawai kufanyika nchini imefahamika
Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' ameliambia gazeti hili kwamba utafanyika kesho jumanne Desemba 8, katika ukumbi wao wa Amana uliopo Ilala
Alisema katika uzinduzi huo bendi ya African Star wana wa 'Twanga Pepeta' yenye mashabiki lukuki nchini watawasindikiza ndugu zao wa Msondo
Akielezea maandalizi zaidi Mhamila alisema licha ya kusindikizwa na bendi hiyo pia wamejipanga kutoa zawadi kwa mashabiki wao, ambapo kila mpenzi atakaekata tiketi ya kuingia ukumbini atapewa zawadi ya albam yao mpya,
Alisema nyimbo zitakazotambulishwa siku hiyo ni pamoja na wimbo uliobeba albam hiyo, Huna shukrani uliotungwa na Saidi Mabera,Kiapo (husein jumbe) aki yangu ipo wapi (Uluka Uvuluge) Mama Cos, uliotungwa na marehemu (Josephe Maina) Albino (Juma Katundu) Machimbo Isihaka Kitima dj papa upanga) na Cheo ni Dhamana (Eddo Sanga)
Aidha aliwataja wanenguaji watakaokuwa wanatoa burudani katika safu hiyo kuwa ni Amina Said 'quen Emmy' Nacho Mpendu 'mama Nzawisa' na Amiri Saidi 'Dongo' aidha rapa wa bendi hiyo Romani Mng'ande 'Romario' atawachenguwa mashabiki watakaofika katika onesho hilo wakiongonzwa na mkurugenzi wa bendi hiyo Muhidini Gurumo

Wanamuziki wa bendi ya msondo ngoma wakitoa burudani wakati wa michezo mbalimbali ilioyowakutanisha waandishi wa habari jana kushoto ni Roman Mn'gande Romario na Hamisi Mnyupe.(Picha na Rajabu Mhamila)

Kapteni wa timu ya busines time Elasto Stansalaus akipokea kikombe cha ubingwa wa volebol wakati wa mashindano yaliyowakutanisha waandishi wa habari na kampuni ya BTL kuibuka mshindi wa jumla wa mwaka 2009.(Picha na Rajabu Mhamila)

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni mbalimbali za vyombo vya habari, wakiburudika na burudani za msondo ngoma zilizokuwa zikitolewa wakati wa michezo mbalimbali ilioyowakutanisha waandishi wa habari jana.(Picha na Rajabu Mhamila)

Teddy
Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuniya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda (kushoto) akiwapa mahelekezo warembo wanaowania taji la mimi kisura najitambua walipotembelea kampuni hiyo.(Picha na Rajabu Mhamila)

No comments: