22.11.13

Saturday, January 02, 2010

DJ CHOKA PRESENT THE HOTTEST MC 2009.

Anaitwa Rashid aka Chidi Beenz, nimsanii wa bongo fleva na mwaka jana ndio msanii aliyefanya kollabo nyingi sana na wasanii wa hapa kwetu na nje ya Tanzania.
Kulikuwa na shindano la kumtafuta msanii yupi atakuwa hot kwa mwaka jana na Chidi alikuwa anashindana na wasanii wenzake ambao ni FID Q, MWANA FA, PROF JAY, AY, JAY MOE, LORD EYES, MANGWEAR na JOH MAKINI.

Na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:-
1. Chidi Beenz - 157
2. Fid Q - 133
3. Joh Makini - 132
4. Mangwear - 100
5. AY - 73
6. Mwana FA - 55
7. Prof Jay - 45
8. Jay Moe - 43
9. Lord Eyes - 35

Haya ndio maneno ya Chidi Beenz baada yakumwambia umeshinda "Duh nashukuru tu na nawapenda sana tuko pamoja na nakuja na kitu kinaitwa La Familia NWO. Hata wafanyaje itashindikana kunifikia, Chidi aka Big Boss aka King Kong aka CHUMAAH."

Shukrani kwa wote walivote...nyie ndio mnaousimamisha mziki huu wa bongo fleva
Mungu ubariki mziki wetu wa Bongo Fleva.

No comments: