22.11.13

Saturday, May 08, 2010

Exclusive SMS kutoka kwa AFANDE SELE.


“Hivi sasa kila mtu anajidai anaijua Bongo Fleva kuliko hata wajuzi na wazoefu wa game hili, Bongo Flava inakua upande wa uimbaji lakini marapa wapya hakuna anayeishika jamii. Wengi wana mashairi dhaifu sana na idea ni za kitoto.

“Wengi wanabebwa na ma-Dj wenye maslahi nao. Kuna Ma-Dj wanawaumiza makusudi wakongwe hata kazi zao za ukweli wanazibana wakidhani wanaua wakongwe kumbe wanaliua game zima. Wanakata nguzo kuu ambazo ni mashairi na ujumbe bora toka kwa wakongwe ambao wanatambua haki zao.

“Walionyonywa ni wengi, wanaharakati wa ukweli! Sasa jamii inapaswa kuamka na kudai kile cha ukweli na si kuamini kila wanachokisema ma-Dj walioanza kazi juzi wakati game imetolewa mbali tena kwa machozi, jasho na damu.

“Watu wanapaswa kujua kwamba Watanzania ni walewale na si wajinga kama baadhi ya Ma-Dj na watangazaji wanavyofikiri kuwa kila wanachotaka wao basi Wabongo wataamini. Leo hii kuna artists wanapewa promo kila siku kwa kulazimisha lakini bado ukija huku mtaani watu bado hawawajui kwakuwa mchango wao katika game haufanani na sifa wanzopewa.

“Shabiki wa Afande, Prof. Jay, Daz Nundaz ndiyo huyo huyo atakayemkubali na artist mpya anayetoka vyema katika game, sasa kama kutoka kwa wasanii wapya dhaifu ndiyo kunasababisha kuwaua wakongwe wa ukweli, basi mashabiki hawatoendelea kuamini game na matokeo yake hadhi ya muziki inashuka.


Habari hii inaendele..ingia hapa ili kumalizia msg hii iliyotumwa na Afande Selle a.k.a Baba Tunda.

http://abdallahmrisho.blogspot.com

1 comment:

Anonymous said...

Wapiii, wasanii wa fleva wote ni useless tu. Tusidanganyane hapa!