Me naitwa P-Shawn kwa jina la kisaniii...nilishafanya ngoma na Ziggy Dee inaitwa "MAISHA" mwaka 2007 na ilifanikiwa kuingia hadi kwenye top 20 za EATVTOP 20 na kufanikiwa kushika namba 6...kuna nyimbo nyingi tulifanya wakati huo na producer alikuwa Washington kutoka Uganda anayefanya ngoma nyingi zikiwema za Bebe Cool, Cindy na hata Salary ya Nameless!!!kwa kuwa nilirudi nyumbani na kuachana na maswala ya kufanya muzik nadhani niwapatie wadau hii nyimbo...inaitwa "Tutakukumbuka" artist ni mimi P-Shawn, Ziggy Dee, Washington na Jo Stan...Producer ni Washington na imefanywa katika Studio ya Ziggy Dee inaitwa Livewire Records ilikuwa inapatika katika maeneo ya Bunga Jijini Kampala..Kwa sasa Ziggy bado anafanya Music, Washington ni Bonge la Producer kama unafuatilia music ya Uganda utakuwa unasikia mikono yake ya kutosha sanaaaaaa,,,Jo Stan ni mtu wa Morogoro kwa sasa ameokoka na mimi nimeacha music kwa muda na sidhani kama nitarudi kunako game tenaa.......Haina maana kukaa na hizi nyimbo ndani wakati kuna watu wanapenda kuzisikiliza soo mafan wa blog yako na watu wote wenye nia ya kuicheza waicheze popote wakiona inafaa. Me ndiye nimechana, Stan na Washington wameimba kiingereza Ziggy kapiga Kibaganda...Ebwana me ni Mtanzania kabisaa na aliyeimba Versey ya kwanza ya kiingereza ni Mtanzania pia....then unaweza mcheck ngwea coz ni binamu yangu kwa sasa niko Sumbawanga na Jo Stan ambaye ni Mtz aliyeimba versey ya kwanza yuko morogoro kule tulikuwa tunasoma tu chuo
1 comment:
....Ebwana huyo dogo namkumbuka nilishawahi kuhudhuria shoo yake na Zig wakati niko Uganda miaka fulani ya 2007 but mbona amechana hivyo! Ebwana dogo anaweza na kwa nn analicha gemu wakati yuko vizuri km vp agonge hata reggae mzee! Big up sana mana hili goma nalifeel sana!
Post a Comment