22.11.13

Monday, October 03, 2011

Miss Jestina Blog Kuwania Tuzo ya Blogu ya Mwaka 2011...!!!

MISSJESTINAGEORGE.BLOGSPOT.COM imechaguliwa kuwa mojawapo ya blogs ambazo zitakazo chuana vikali katika kuwania ushindi  wa kutafuta BLOG ya mwaka katika tuzo za BEFFTA (Black Entertainment Film, Fashion, Television and Arts) zitakazofanyika tarehe 22 Octoba 2011 hapa jijini London.
Kwa heshima na taadhima zote naomba wadau tuipigie kura ili blog yetu iweze kupata tuzo hii muhimu. Hii ni Blog pekee kutoka Tanzania  kuingia katika kinyang'anyiro hiki. 

Jinsi ya kupiga kura ni rahisi tu tembelea www.beffta.com/voting utaona fomu ya kujaza andika jina lako, email yako, halfu chini ya Category chagua News 4. Blog of the Year na kwenye Nominee  chagua Miss Jestina George <http://www.missjestinageorge.blogspot.com
>. Baada ya hapo bofya Submit Your Vote.
Blog ya www.missjestinageorge.blogspot.com ina husika na Mambo ya Urembo, Mitindo, Sanaa na Matukio Mbalimbali na Motomoto kutoka kila pande za dunia.
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wale wote ambao watakaoweza kunipigia kura na hata wale wambao hawata weza kunipigia kwa sababu moja au nyingine.
Asanteni sana na wote Mbarikiwe.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Wabariki Watanzania

No comments: