Baada ya Mbatizaji a.k.a Sauti ya nyikani akiwa amemshirikisha mtayarishaji wa Muziki hapa nchini Tanzania,Man Water kuweza kutoa Wimbo ujulikanao kwa jina la Heshima Kazi,ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio hapa nchini,tayari amekamilisha video ya wimbo huo,akiwa ameifanya chini ya kampuni ya SHOWBIZZ DEFINE VIDEOS,chini ya mtayarishaji Eryne Epidu.Picha za wimbo huo zilipangwa kupigwa maeneo tofauti tofauti ya kigamboni,jijini Dar es salaam kwa mujibu wa Mbatizaji na Man water,lakini muaandaji wa wimbo huo,ama producer wa video hiyo baada ya kuusikiliza wimbo huo alikuja na wazo jipya na kuamua kushoot picha za wimbo huo maeneo ya Feri na maeneo ya Posta jijini dar es salaam.Video itakuwa pouwa kwa sana,kama vipi tega macho yako katika luninga na mtandao huu utaiona Heshima kazi hivi punde.
No comments:
Post a Comment