MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha Mapinduzi, mkoa wa Iringa,
Ritha Kabati, ameshirikiana na washindi 20 wa ‘Kabati Katiba Star Search’ kutoa
kibao kipya cha Muziki wa Bongo Flava kiitwacho ‘Iringa Bila Ukimwi
Inawezakana’, .
Kibao hicho alichorekodi na
wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya walioibuka washindi wa shindano
hilo la kusaka vipaji, umerekodiwa katika studio za Top Magic Sound chini ya
mtayarishaji wake mahiri Ecko
Wimbo huo ni harakati za
mbunge Kabati alizozianzisha katika kuwakomboa vijana katika majanga na makundi
hatarishi kama ya uvutaji wa bangi, ngono zembe zinazochangia maambukizi ya
ukimwi – ugonjwa ambao kwa mujibu wa takwimu za mkoa huu unaongoza kwa maambukizi
mapya.
Akiunzungumzia wimbo huo,
Kabati amesema anaimani ujumbe uliomo utaifanya jamii kubadilika na hatimae
kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi mkoani iringa na taifa kwa
ukjumla.
WIMBO-IRINGA BILA UKIMWI
INAWEZEKANA
ARTIST-KABATI ALL STARS
STUDIO-TOP MAGIC SOUND
IRINGA
PRODUCER-ECKO
No comments:
Post a Comment