Mambo vp ndugu zangu.
Napenda
kuchukua nafasi hii kuwatakia maandalizi mema ya mwaka mpya. Mungu atupe nguvu
na neema zaidi ktk mwaka 2013. Mwaka 2012 tutaukumbuka kwa mengi yapo mema na
mabaya. Naomba nikuombe radh wewe kwa lolote ambalo niliwah kukukosea, nawe
kama ulinikosea sina tatizo nawe tangu sasa. pia naomba nitoe shukrani zangu
kwa wote waliohusika ktk mafanikio yangu ya kimuziki. Naamini wengi mlikuwa
mstari wa mbele ktk kunishauri, kunipongeza nahata kunikosoa nilipokosea.
Shukrani nying zwafikie radio presenter, dj's, radio na tv zote tz na Afrika
naamini bla nyinyi kuzicheza nymbo zang Basi nisingefika hapa.
Waandaz wa
magaazeti mlikuwa mstari wa mbele ktk kuona nafika mbali kwa kuandika habari
zangu na kufika hata vjijini. Nachukua fursa kuwashukuru pia. Blogs mbalimbali.
Mlikuwa mstari wa mbele kwakuandka habari na kupost hata baadh ya show zangu
ambazo mmenipa heshma ya kufika mbali zaid na kusikika hata nje ya nch mchango
wenu ni mkubwa japo siwez kuwataja wote. Pia Requester wa media cna cha
kuwalipa nawashkuru sana sana na ntabaki kuwaheshmu kwani mmetoa mchango mkubwa
sana kwa kuomba nymbo zangu media na zikachezwa Na amini ni mchango mkubwa sana
ktk game hasa kwetu wasanii Ntabaki kuwaheshimu na kuwathamini siku zote. Bila
kuwasahau wasanii wenzangu walikuwa nami bega kwa bega ktk kunishauli na
kunisaidia kwa chochote.Pia ma dj wa club mbalimbali, mmekuwa chachu ya mzk
wangu pale mlipoonesha ushirikiann wenu kwangu.
Pia Waandaaji wa (show)
matamasha madogo na makubwa nawashukuru sana sana kwa kuniamini na kukubali
kufanya kazi na mm Siwasahau maproducers wa video na Audio na studio mbalimbali
kwa kunifanyia kaz za uhakika na jamii ikanikubali kwa kazi hzo. Wote kwa
pamoja naamini sasa ni kama ndugu. Nawaomba muonyeshe tena moyo huwo na mwaka
ujao na mingine kwani kaz nzur ni yenye kushirikiana. Msisite kama ntawakosea
naomba msisite kunikanya na kunisamehe. Napenda wote na kuwajali. Nawatakia
mwaka mpya.
Ts me. Dayna Nyange (mkali wao)
No comments:
Post a Comment