Msanii kutoka Kenya aitwaye Pewa Abagenge,inaonekana
hajamaliza beef yake Na Godfather wa Genge(NONINI),katika wimbo wake mpya ambao
ameutoa wiki hii anasikika akikashifu ma presenter ambao pia ni wasanii.Nchini
Kenya wasanii wengi chipukizi wamekuwa wakilalamika kwamba presenter ambao pia ni wasanii hawachezi
ngoma zao kwa kuogopa competition,Hii inajidhihirisha sana kati ya Pewa Na Nonini,kwani
wanafanya mziki aina moja na la kustajabisha ni kwamba mziki wa Pewa hauchezwi
kamwe kati show ya Nonini na pia FM ambako Nonini anafanya kazi yake.Nikinukuu
kutoka kwa wimbo wenyewe amesema
“Hii sanaa ina
Ufisadi inashinda hata serikali,
Promo ngoma mbaya
,wanakanyagia kali,
Presenter ni msanii
anaogopa competition
Kwa jina la Baba
mi nakemea roho chafu”
Katika wimbo huu pia amemtaja Huddah Monroe,binti aliyekuwa kwenye
BBA ya mwaka huu wa 2013 na kuondolewa baada ya wiki moja,amekashifu tabia
potovu ambazo mabinti wa Kenya akiwemo Huddah,
Sidika na wengineo Wameingilia huku wakijiita socialite ilhali ni utovu wa nidhamu,huku
akimsifu Kethi, binti wa aliyekuwa Seneta Wa Makueni Nchini Kenya kwa ushujaa
aliouonyesha wakati wa Kesi ya Urais nchini Kenya.Wale waliouza nafsi zao ili
wawe mabingwa kwa industry pia hawajaponea kukemewa na msanii huyu,hapa
inaonekana anamwashiria gwiji wa hiphop Octoppizzo
na wasanii wengine wanaojulikana nchini Kenya walioko katika dini la Free
Mason.
Jambo lingine pia hajakosa kunena kuhusu
mabinti wakenya waliopatikana wakishiriki porn na mbwa mjini Mombasa,Pia maovu
yanayotendeka serikalini,anasikika akisema “
Wengi wameuliwa
Kesi Zao mahakamani,
Tume za uchunguzi
ni miradi ya serikali,
Kesi imelipiwa
mwenye kesi haonekani,
Kwa jina la baba mi
nakemea Ufisadi”
Wimbo huu kwa hakika utawagusa wakubwa walioko kwenye
serikali pia wadogo mitaani,
SIKIZA
WIMBO WENYEWE UTOE UAMUZI WAKO MWENYEWE. Katika wimbo huu
amemshirikisha Jokay,msanii
chipukizi toka tanzania
Nakemea –Mistari
Pewaaaa
Abagengeeeee
Jokay…. Eeeeeeh
Kusini Recordz………………
Hii
sanaa ina Ufisadi inashinda hata serikali,
Promo
ngoma mbaya ,wanakanyagia kali,
Presenter
ni msanii anaogopa competition
Kwa jina la Baba mi nakemea roho chafu
Its
only in Nairobi Kahaba anajiita socialite,
No
Love for Huddah,Sidika ameonyesha uchi,
Mwanamke
ni akilia makofi napigia Kethi,
Kwa Jina LA Baba mi nakemea
ukahaba,
Wasanii
wanauza nafsi ngoma zao ziingie chati
Swaga
Ni Bandia wanajiita Illuminati,
Sikiza
ngoma zao wanasifia shetani,
Kwa jina la baba Nakemea Free
Mason.
Miujiza
Kanisani mi ndio Pastor Njoroge,
Imani
ni Lazima geuza mdomo kama mwende,
Gospel
biashara shetani anapigwa Teke,
Kwa jina La Baba mi nakemea
ma hypocrites.
Yote nayoyaona unfair leo nayakemea,
Inanibidi kusema ila wengine watanielewa vibaya*2
Wakenya
ni Wazembe wanalaumu serikali
waiting
for Kenyatta awabaie makali,
Stress
inawamaliza wana Rwanda kaa Kigali,
Kwa jina la baba mi nakemea
mauzembe,
Mombasa
ni sodoma gomorah mi inanitisha
Alikuwa
mlinzi siku hizi anafanya mapenzi,
Naongelea
mbwa dada zangu mnakosea,
Kwa jina la baba mi nakemea
immorality
Mapenzi
ni kaa maua bt siku hizi yananyauka,
Wachache
wanapenda wengi roho zinavunjika,
Mwanamke
ni wako kwa rafiki yako anamegeka
Kwa jina la baba mi nakemea
ma player,
Giza
Nairobi Kenya Power kuna Nuru,
Biashara
niya mshumaa wakenya wanalipa ushuru,
Faida
mnapata but wenzetu inatudhuru,
Kwa jina la baba mi nakemea
monopoly
Yote nayoyaona unfair leo nayakemea,
Inanibidi kusema ila wengine watanielewa vibaya*2
Wengi
wameuliwa Kesi Zao mahakamani,
Tume
za uchunguzi ni miradi ya serikali,
Kesi
imelipiwa mwenye kesi haonekani,
Kwa jina la baba mi nakemea
Ufisadi
Mtoto
wa miaka kumi mja mzito miezi tisa
Nani
mtamlaumu saa wazazi washalegeza
Ngono
mtaani siku hizi mchezo wa kuigiza
Kwa jina la baba mi nakemea
mafisi
Wengi
wamesoma wamepata degree
Ndugu
yako ndio kazi karatasi haisaidii
Wanjala
kimani musyoka na otii
Kwa jina la baba mi nakemea
ukabila
Siasa
ni siasa wanasiasa ni siasa
Nguruwe
atakula bt hakuna siku atasaza
Kweli
ni ukweli basi fight on ALAI
Kwa jina la baba mi nakemea tama
Yote nayoyaona unfair leo nayakemea,
Inanibidi kusema ila wengine watanielewa vibaya*4
No comments:
Post a Comment