Jimmy Master
YULE muongozaji na mwigizaji Jimmy Mponda 'Jimmy Master' aliyetikisa
na mfululizo wa filamu za misuko iliyotoka sehemu ya kwanza hadi ya
tatu na baadaye kujiongezea jina lingine akiitwa J Plus.
Kwa sasa nyota huyo amefunguka kuwa yukombioni kutoa muvi ya mwisho
inayoitwa Doble J Final huku ujio huo ukiwa ni wa mwisho kutoka baada
ya kutangulia na Doble J sehemu ya kwanza na yapili zilizotoka mwaka jana.
"Mwaka jana nilifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa filamu hususani
wanaopagawa na filamu za mapigano na kujawa mambo ya kipelelezi,"alisema J Plus.
Alisema Doble J Final pia ni ujio wake wa filamu nyingine ya mapigano na
kuna heka heka za kipelelezi ndani. J Plus aliyezoeleka sasa katika kuonesha
ubabe wa kufa mtu , kwa sasa ujio wake huo unao tazamiwa kuingia sokoni mapema tu ,
mwezi ujao .
Pia Jimmy Master amemshirikisha mbabe mwingine katika filamu za mapigano Ibrahim Mbwana 'Bad Boy'
na pia wamo nyota wengine katika dulu la filamu kama Charles Magari , Hashim Kambi na
Veronica Viankero.
No comments:
Post a Comment