Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ali Abdalla Ali (mwenye
kofia)akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa
Nje wa Vodacom Salum Mwalim kwa ajili ya timu ya mpira wa miguu na wa
pete za Baraza la
wawakilishi. Vodacom imezipatia timu hizo jezi, suti za michezo, viatu
na mipira vikiwa na thamani ya Sh 4.5Milioni. Wanaoshuhudia ni Meneja wa
timu Nassor Salum Aljazera(kushoto) na Meneja wa Vodacom Zanzibar
Mohamed Mansour.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ali Abdalla Ali (mwenye
kofia)akipokea mipira ya soka na pete kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Nje
wa Vodacom Salum Mwalim kwa ajili ya timu za baraza la wawakilishi.
Vodacom imezipatia timu
hizo jezi, suti za michezo, viatu na mipira vikiwa na thamani ya Sh
4.5Milioni.
Kutoka kushoto: Meneja wa Timu za Baraza la Wawakilishi Nassor Salum
Aljazeera, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Naibu Spika
wa Baraza la Wawakalishi Ali Abdala Ali, Meneja wa Vodacom Zanzibar
Mohamed Mansour, Makamu
mwenyekiti wa Michezo Baraza la Wawawakilishi Mbarouk Mtando na Mweka
Hazina wa Baraza Dau Maulid kwa pamoja wakionesha vifaa vya michezo
vilivyotolewa na Vodacom kusaidia timu za baraza.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiteta jambo na Naibu
Spika wa Zanzibar Ali Abdala Ali na Meneja wa Timu za Baraza la
wawakilishi Nassor Salum Aljazeera ambae pia ni Mwakilishi wa jimbo la
Rahaleo wakati wa hafla fupi
ya kupokea vifaa vya michezo vilivtolewa na Vodacom kusaidia timu ya
soka na mpira wa pete za Baraza.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiongea wakati wa hafla
ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na Vodacom kwa
timu za Baraza la Wawakalishi iliyofanyika ofisi za Baraza hilo Mjini
Zanzibar. Kulia ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar
Kheri na Naibu Spika wa Zanzibar Ali Abdalla Ali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar
Kheri akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo
vilivyotolewa na Vodacom kwa timu za Baraza la Wawakalishi iliyofanyika
ofisi za Baraza
hilo Mjini Zanzibar. Wengine pichani ni Naibu Spika wa Zanzibar Ali
Abdalla Ali(katikati) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum
Mwalim.
Kampuni
ya Vodacom Tanzania imekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili
ya timu za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ili kuzipiga tafu
timu hizo kushiriki kwenye mashindano ya urafiki mwema yanayotarajiwa
kufanyiaka jijini Arusha mwishoni mwa mwezi huu.
Vifaa
hivyo ambavyo ni seti mbili za jezi kwa kila timu ya soka na ya mpira
wa pete, mipira, viatu, soksi na suti za michezo vikiwa na thamani ya
zaidi ya Sh 4 Milioni vimepokelewa leo na Naibu Spika wa Zanzibar
Ali Abdala Ali kwenye hafla fupi iliyofanyika ofisi za Baraza la
Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Akipokea
vifaa hivyo Naibu Spika Ali ameishukuru Vodacom kwa msaada huo
alioutaja kuwa ni silaha nzuri itakayoziwezesha timu za Baraza kushiriki
vema na kwa kujiamini kwa kile alichokifananisha na nondo kwenye
ujenzi wa nyumba.
“Vodacom
mmetupatia nondo za michezo kwa kuwa kama ilivyo kwenye ujenzi wa
nyumba nondo ni kifaa muhimu vivo hivyo nondo za kwenye michezo ni vifaa
bora hivyo hatuna budi kuwashukru (Vodacom) kwa dhati kabisa
kwa msaada huu.”Alisema Naibu Spika
Naibu
Spika Ali amesema timu za Baraza la Wawakilishi zimekuwa kwenye uhitaji
wa vifaa kuhakikisha inakuwa na ushiriki mzuri kwenye mashindano
mbalimbali ikiwemo ya hivi karibu ambayo ni ya Arusha itakayoshirikisha
timu mbalimbali zikiwemo za Mabunge pamoja na mashindano ya maadhimisho
ya miaka hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema
msaada huo sio tu kwamba umelifurahisha Baraza la Wawakilishi bali
Serikali na Wazanzibari wote kwa ujumla kwa kuwa unaonesha muendelezo wa
kazi nzuri na kubwa inayofanywa na Vodacom katika kusaidia jamii
hapa Zanzibar.
“Tumefarijika
sana na msaada huu tumekuwa mashuhuda na wenye kusikia kazi za kijamii
mnazozifanya hapa Zanzibar na leo mnageukia michezo hili linamfurahisha
kila mmoja na kwa niaba ya Baraza na wadau wengine wote
tunawashukuru.”Alisema Naibu Spika na kuongeza kuwa “Mmetuwezesha
kwenda Arusha na sasa tunawaomba (Vodacom) muangalie jinsi mtakavyoweza
kusaidia timu zetu hizi na maeneo mengine tunapoelekea kwenye
maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.”
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Haji Omar Kheri ambae pia ni Mwenyekiti wa Wawakilishi Sports Club
amesema Zanzibar inatambua kazi kubwa Vodacom inayofanya kusaidia
jamii na hivyo kuifanya kampuni hiyo kuwa moja ya kampuni kubwa zaidi
hapa nchini.
Vodacom
ni moja ya kampuni kubwa za kibiashara hapa nchini mmejiunga vizuri na
mmekuwa na kazi nzuri za kuboresha huduma zenu lakini kipekee
tunafurahishwa na kazi zenu za kusaidia jamii hapa nchini……. Na kwa
upande wa hivi vifaa tumevipokea kwa furaha kubwa”
Akizungumza
kabla ya kukabidhi vifaa hivyo Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom
Salum Mwalim amesema Vodacom inatambua nafasi ya viongozi wa kitaifa
wakiwemo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika kushajiisha
ajenda za maendneleo ikiwemo michezo.
Mwalim
amesema kuwa Vodacom inaamini kuwa kasi ya ushiriki wa Wawakilishsi
kwenye michezo ni chachu katika kuinua kiwango cha michezo mjini
Zanzibar.
“Vodacom
tunatambua umuhimu wa nyie (Wawakilishi)kushiriki katika michezo jamii
inapowaona mkiwa katika mstari wa mbele kwenye michezo bila shaka nao
wanahamisika na kushiriki michezo na kwa njia hiyo basi tunajenga
afya zetu, tunaimarisha udugu na mshikano na kujenga urafiki na nchi za
nje.”Alisema Mwalim
“Kote
mtakapopita kuelekea Arusha wananchi watawaona na kupitia kwenu ujumbe
wa michezo utaenea na hivyo kuendeleza michezo.”Alisema
Kazi
ya kukuza michezo haiwezi kuachwa kwa Serikali na ZFA (Chama Cha Soka
Zanzibar) pekee ila ni jambo linalohitaji wadau kujitokelea na kutumia
utashi wa kisiasa wa michezo mlionao kuisadia Serikali na ZFA kurudisha
enzi tukufu za michezo zilizowahi kuwika Zanzibar katika miaka ya
themanini na tisini.”Aliongeza Mwalim
Mwalim
ameziomba timu za Wawakilishi kutumia msaada huo kama chahu ya kufanya
vema na kurudi na ushindi kutoka mashindano ya Arusha huku pia
ikijipanga vema kwa mashindano ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi
matukufu ya Zanzibaryatakayozishirikisha timu za mabunge ya Afrika
Mashariki.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment