Mwanamitindo wa kimataifa
wa Tanzania, Millen Happiness Magese amewataka watu binafsi na makampuni
mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika kusaidia tasnia ya elimu hasa katika maeneo
yasiyopewa kipaumbele ili kuwaokoa watoto wa maeneo hayo kutotumbukia katika
vitendo visivyo vya kimaadili. Rai hiyo ameitoa wakati alipotembelea miradi
yake aliyoifadhili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na utengenezaji wa
madawati.
Ujenzi wa madarsa
unaendelea katika shule ya msingi Mjimwema iliyopo manispaa ya Mtwara ambapo
mradi wa kutengeneza madawati ulikabidhiwa kwa vikundi mbalimbali vya
wajasiriamali mkoani hapo kwa mpango maalum kupitia ofisi ya mkuu wa Wilaya,
Mheshimiwa Wilman Ndile. Jumla ya madawati hamsini na tano (55) yenye thamani
ya shilingi milioni tano yalikuwa tayari yameshatengenezwa kama walivyoahidi
wajasiria mali hao wakati wakikabidhiwa kazi ya utengenezaji wa madawati hayo.
Madawati hayo
yalikabidhiwa rasmi na Millen yalikabidhiwa kwa wanafunzi wa shule ya msingi
Lilungu.
Kwa upande wa afisa elimu
wa manispaa ya Mtwara Frola Aloys amewataka wadau wa elimu kuonesha uzalendo wa
hali ya juu kwa maeneo ya Kusini mwa Tanzania huku mkuu wa shule ya msingi
Lilungu Abdul Nangomwa akielezea changamoto zinazoendelea kuikumba sekta ya
elimu katika shule za msingi wilayani Mtwara.
Mbali na kukabidhi
madawati Millen aligtembelea ujenzi unaoendelea shule ya msingi Mjimwema na
kutoa zawadi ya madaftari napenseli kwa wanafunzi hao ambapo mpaka sasa shule
in mikondo mitatu ambayo ni kuanzia darasa la awali mpaka darasa la pili.
Ziara hiyo ya mrembo huyo
aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania mwaka 2001, ni mwendelezo wa shughuli
za kijamii anazozifanya nchini Tanzania hasa katika kusaidia makundi yenye
mahitaji maalumu na yale yasiyopewa kipaumbele.
Mwinzoni mwa mwaka huu
Millen Magese alitoa kiasi cha shilingi milioni kumi na tano katika kusaidia
huduma hiyo ya elimu katika manispaa ya Mtwara.
Mwisho.
Kwa maelezo zaidi
wasiliana na:
Tabasamu PR Consultancy,
+255 754 602 674.
No comments:
Post a Comment