22.11.13

Wednesday, June 09, 2010

KATIKA PITAPITA ZANGU JIONI HII YA LEO.

Hiki kibajaji nimekutana nacho leo maeneo ya Bamaga kimeandikwa hivi kama unavyoona hapo nyuma. Huu ni msemo uliopo kwenye nyimbo ya Prof Jay. Je wadau kuna ulazima maneno ya wasanii yakikutwa yametumika kwenye sehemu za biashara kutozwa hela kwa muhusika wa sehemu hiyo

Baada ya hapo nilipofika maeneo ya Kijitonyama Sayansi wakati nasubiri niingie kulia kwangu nilimshuhudia Trafik akiongoza magari huku akiongea na simu yake ya mkononi.
Je ni sahihi.

8 comments:

Anonymous said...

kwa sababu yeye ni mwanadamu kama walivyo wengine na anahitaji mawasiliano, haina tabu, kwa mfano wewe hujawahi kupokea simu ukiwa unaendesha gari?

Anonymous said...

kuhusu bajaji, sidhani kwani si sahihi kwa sababu ni neno la kiswahili, ila kama ingekuwa inatumika kama wimbo au sauti ya muhusika hapo sawa, tufanye mfano maneno yote ya kiswahili yatumike na wasanii itakuaje? haitawezekana kwani hata yule aliyegundua 'mambo' au Mchungaji Mtikila aliyevumbua neno la WALALAHOI angehitaji malipo kwa kila anayelitumia, thanks mdau kwa chalengi

Anonymous said...

Choka... Kuhusu suala la kutozwa hela kwa maneno yanayotumika katika sehemu za biashara kwa madai eti ya wasanii itakua ngumu sana sababu hakuna ushahidi wakuwa yeye ndio ameanzisha neno hilo.. sikubali kwamba Prof J ndio alikua mtu wa kwanza anayezungumza kiswahili duniani kuuliza 'Hapo vipi?' na kama kwa sababu ni nyimbo mbona kuna nyimbo kibao zinafanana majina lakini hakuna anayemlipa mwenzie ila labda kama mtu ameiga mistari na siyo jina la wimbo.
kuhusu Askari wa usalama Barabarani ni sahihi kupokea simu kwa sababu pengine anajulishwa avute gari za line fulani kwa sababu kuna msafara wa kiongozi au anajulishwa kuna gari aina fulani yenye namba fulani imefanya kosa na inaelekea pande hizo hivyo aikamate ikifika hapo.
Ni mtazamo wangu tu...

dogo said...

mkuu hakuna ulazima coz hayo ni maneno tu ambayo yalikuwepo, sema tu yalikua hayatumiki kivile ila baada ya wasanii kuyatumia kwenye nymbo zao ndo nayo yakashika kasi so ukisema hivyo yalipiwe kwa wale waanzilishi basi TUKI wangetudai maneno mengi sana tangu walipoanza kusanifisha lugha hii ya kiswazi mzee, mi nilikua naomba tu waache watu wayatumie bila ya kutozwa hela kwani kwa kufanya hivyo lugha yetu inakua mzeeyaaaa,pia leo katika soma soma yangu hapa chuoni nimeona maana ya neno nyimbo kuwa ni lazima iwe na mistali mitatu na kuendelea na maudhui yake zaidi yamejikita katika mapenzi kwa hiyo wale wasanii wetu wa bongo fleva wanaoimba please tuwaache wafanye hivyo na waachwe waendelee kujikita kwenye mapenzi kama ilivyo zoeleka kwani hata maana ya nyimbo imeonesha maudhui yake makubwa ni mambo ya mapenzi tu.
Big up mwana ni mimi, Johnson Matembo wa www.dodjohnson.blogspot.com wa Tumaini university-Arusha second year mzazi taking a bachelor of Linguistics especially on Swahili language.

Anonymous said...

Yeah Choka,dont see anything wrong with that kwani atumii mikono yote miwili kuongoza magari ila ili uwe makini zaidi inahitaji kufanya one thing at a time,ebu nikuulize je nikosa kuendesha gari na mkono mmoja?

Amri Dadi Mkova said...

Niambie Choka..mambo vipi..Mi naona sio lazima kwa wasanii kudai baadhi ya misemo inayotumika na watu kutoka katika "NYIMBO" zao. sababu wasanii wana uhalali na umiliki wa "WIMBO" Mzima na wala si msemo!!!..Pili ningependa sana ubadilishe desturi ya kuita NYIMBO baada ya kuita WIMBO Ikiwa unamaanisha hali ya umoja..Sijui umenielewa hapo..WIMBO ni Umoja na NYIMBO ni Wingi..Wako mfatiliaji namba moja! DEEE

Anonymous said...

huyo polisi inabidi afukunzwe kazi mjinga kupita kiasi, na hayo maneno sio ya wasanii ni maneno ya lugha so yatumike bure kuwacharge watu kwa ajili ya maneno hizo ni njaa za kupindukia na ujinga pia

Anonymous said...

hii sio sawa kabisa trafic anaongea na simu hiyo ni maisha ya watu sio game iyo lazima aweke akili yake yote kwenye kuongoza magari sio kuchanganya mambo hizi ni risk ambazo zinaweza leta hasara ya maisha ya mtu ndo maana bongo watu wanakufa kizembe sababu ya kuweka vitu muhumu kuwa simple hii sio professional anywhere in the world