22.11.13

Tuesday, June 22, 2010

NEW ALBUM YA JCB.

Msanii wa hip hop hapa bongo,akitokea mjini Arusha akijulikana kwa jina halisi la Jacob Makalla a.k.a JCB, hivi karibuni amekwisha ikamilisha albamu yake ijulkanayo kwa jina la Nakala za Makala yenye jumla ya nyimbo 16.

akizungumza leo mchana ndani ya kipindi cha XXL kinachorushwa na redio ya Clouds FM,kupitia mtangazaji wake mahiri kabisa B Dozen,amesema kuwa albamu hiyo iko tayari na imekwishaingia sokoni leo kwa ajili ya mauzo.

JCB amezitaja baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo kuwa ni Movement of silence,Kijiti,Kijenge ya juu,Usinitafute,Prison break,Ninapo,arusha na nyinginezo,anasema na kuongeza kuwa albamu hiyo imerekodiwa ndani ya studio za Watengwa chini ya prodyuza David Bakari a.k.a Daz.

JCB amebainisha kuwa albamu hiyo iliyojaa kila aina ya maudhui inauzwa buku kumi tu.Ukiitaka basi wasiliana nae kwa namba yake ya kiganjani

0713 641677 au 0784 641677

Habari kutoka kwa Michuzijr

No comments: