Detour of Real Love ama Njia Ndefu ya Penzi la Dhati ni tamthilia mpya ya radio ambayo imeandaliwa kwa ufundi mkubwa kuwapa burudani wapenzi wa radio wenye hamu ya kupata drama yenye mfumo wa filamu kupitia radio.
Tamthilia hii inamhusisha kijana handsome aitwaye Ian ambaye anapata mkate wake wa kila siku kwa shughuli ya ukonda wa daladala. Katika kazi zake za kila siku anakutana na dada mrembo, msomi na mtoto wa tajiri aitwaye Rachel ambaye anapanda daladala hiyo akiwa na mpenzi wake Erick ambao wanasoma chuo kikuu. Upole, werevu na mvuto alionao Ian unampagawisha Rachel na kumfanya afanye kila aliwezalo kumpata kijana huyo bila kujali tofauti zao za maisha. Baada ya Erick kunyang'anywa mpenzi wake na konda Ian, anaamua kulipiza kisasi kwa kuwawinda wapenzi hao wapya. Furaha fupi na ahadi aliyoipata Ian kwa kupendwa na Rachel inadumu kwa muda mfupi na kuyaona maisha kama jehanamu.
Detour of Real Love imeandikwa na mwandishi anayekuja juu Tanzania aitwaye Victor Chuma na kutayarishwa na Fredrick "Skywalker" Bundala. Muziki katika tamthilia hiyo umetayarishwa na Skywalker na Amba produsa kutoka Iringa.

1 comment:
Ni kila siku za jumatatu kuanzia saa 5;00 usiku na kurudiwa Jumapili saa 6:00 Usiku kupitia Radio Free Africa.
Post a Comment