22.11.13

Monday, June 07, 2010

USIJE MJINI RMX KUTOKA KWA MTOTO WA? VITOTO.

Kama ningekua msanii na nnataka kutoka, ningefanya hiviiiiii

"NAKUJA MJINI"
Chunga mifugo yako isile mazao yangu....Moja ya nembo maarufu hapa kwetu kijijini...
Nipo zangu ndani ya basi,mi nakuja huko mjini.
Nimekaa sina wasiwasi,ukiniona hutoamini.
Mi ni mtoto wa kiume,natafuta najiamini.
Sina budi nijitume,sasa kwanini nisije mjini?
Haijalishi ukinitisha,kwamba mjini sio kuzuri.
Tamaa huwezi kunikatisha,haso kwangu ni desturi.
Mbunge wetu mwache,huko huko alipokuwa.
Zimebaki siku chache,uchaguzi utamuumbua.
Maendeleo yanachelewa,siwezi baki niyangoje.
Kidume siwezi letewa,nakuja huko nijionee.
Eti wamasai hawachungi ng'ombe?,ni sawa walivyoacha.
Mjini hakuna ng'ombe,vipi wafanye anasa?
Umesema kuna manyoya? ngoja nikija ntayanyonyoa.
Watoto wazuri kama latoya,mi nikija ntawaopoa.
Nimechoshwa na tunguli,nataka nitibiwe na madokta.
Sihitaji kazi nzuri,nipo radhi niwe hata konda.
Popote penye pesa,utapeli haukosekani.
Hilo kamwe halitonitesa,nalijua toka zamani.
Mbona wewe umesoma ulaya,wazungu hawajakukataza?
Nakuja skuonei haya,hata bakora ukinicharazaaaaaaaa......
Nakuja mjini leoooo,,,,ah aha ah haaaaa
Nakuja mjini leoooo................!!!!

Written by
Mtoto wa? Vitoto!!

10 comments:

Ima (The Designer) said...

Daaaaaaaaaa choka mwana kwa stahili hii jamaa atatoka cos songi lenyewe ndo liko ktk chart, mi nilizani Inspector ndo atajibu kumbe Vitoto ndo kawa wa kwanza. hahahahahahahah Mwana F.A unabahati mbaya mwana kila songi lazima ujibiwe.

Unknown said...

such a good creativity,damn i like that verse...ingia studio dogo!!!

Anonymous said...

hiyo verse kali sana kushinda hata ya Mwana FA. da ila the funny thing is, nyimbo anazotoa FA kila mtu anataka kujibu. Mnakumbuka ingekuwa vp, Bado nipo nipo na sasa hii

Anonymous said...

Hee!! hii imekaaa sawa, Jamaa anatunga, si utani, nimependa pale aliposema, " Mbona we umesoma ulaya wazungu hawajakukataza"
na mimi ngoja nikupe verse zangu kukujibu


anyway angalia isiwe beef. mjini njoo komaa kivyako vyako, l
lakini kuwa makini usije ukaamua kuwa kibaka,
mjini tunakutia kibiriti.. manake tumechoshwa na vibaka.
Mjini sio mchezo, wenzako wanakula bata we unakula ukata.
Mjini kuna dili za kumwaga, lakini pia kuna dili za kifala, kuuza unga, kula unga na kisha kudata.

dogo said...

Daah!!
Kaka mambo vipi pande za huko kidaa daa? sie huku Arachuga tunakomaa tu na baridi kari kama tupo ulaya bwanaaaaa!! so nilikua nataka kujua huyo mtoto wa vitoto anamkubali sana mzee mzima Mwana FA coz nae kafanya kama alivyofanya Inspecta Haruni katioka ile ngoma ya bado nipo nipo so kwa nini asije na idea yake mpya au ndo vile mwana anaendeleza bifu coz namsikia sana clouds akiwa DISS wana huyo mtoto wa vitoto mbona yeye hajawai KUDISSIWA, ila poa mwambie mwana tunataka changam,oto mpya si kuja kurudia rudia tu IDEA ya mwingine. Mwana FA ndo mwana harakati wa ukweli si unaona town mambo yanakaba sana so wakija wote hapo kwa Lukuvi nani atabaki na Babu na Mkewe Bibi???
Poa ni mimi dogo Johnson wa www.dogojohnson.blogspot.com wa Tumaini University-Arusha.
Big up mwana blog imesimama ile mbayaaaaaaaaaaa kip it up!!

Anonymous said...

kwa kwel wa2 ka hawa nawaonaga hawana vipaj mpaka wenzao wa2nge nyimbo ndo wao wawjbu kama wao ni wasanii kwanin wactunge zao??????

Anonymous said...

eBANA daaaah kama ni yeye kweli mtoto wa vtoto ndo kaandika hvyoo basi big up sana kwakee daaah hajakoseaa wala nn daaah Hope dat Binamu! umeooona daah !! katisher ile mbayaaa!

najongea said...

Artist must be creative,but why this underground use to come up with other musicians idea?Look small guy like Justin Barber come with his own idea without imitating others style but now he is everywhere on airtime.
Just try to be creative and not coping,past and vise-verse lyrincs.
By,
Motto
Moscow
Russia.

Anonymous said...

This is 4 Motto frm Russia, who told u kwamba Dogo anataka kutoka soma vzuri Post yake, THIS BOY IS JUST A STAKEHOLDER IN THIS INDUSTRY LIKE OTHERS even u can do it if ur interested with. Cheers homie

NOORDASH said...

Umetishaa