22.11.13

Wednesday, July 14, 2010

NATAKA KUFANYA KAZI KIMATAIFA ZAIDI HAPA MUSIC KULE MOVIES.

Kama dakika 10 zilizopita nilikuwa nachat na msanii wa bongofleva Baby Madaha juu ya ukimya wake nakumuuliza vipi mwanadada huo ubusy unaambatana na nini..? akanijibu
"Yeahh kwa sasa nimetoa New single inaitwa DESPERADO ambayo imetengenezwa na producer Allan Mapigo. Hiyo single itakuwa sound track ya PILIPILI INTERTAINMENT ambayo itaitwa OBSESSION, pia Amore naitengenezea Movie ambayo ita relate na maisha yangu halisi yalivyotokea mpaka nikatunga AMORE, filamu itatoka na video yake"

Nikamuuliza wimbo huo wa Desperado unazungumzia nini haswa, akanijibu
"Kwanza watu wataipenda single ya Desperado kwasababu nimeimba kuhusu upande wa pili wa Mapenzi, unampenda mtu na unampa yote halafu tena hakujali, matokeo yake napata mwingine halafu yeye anarudi tena, hapo ndo inakuwa JIPANGUSEEEE RAAAAH RAAAAH
Gat me?"

Je unalipi la kuongezea na unawaahidi nini mashabiki wako..?
"Napenda kuwaambia mashabiki wangu wote wa Baby Madaha kwamba wakipata nafasi waende Zanzibar kwenye tamasha la ZIFF linaloendelea kwani kuna Filamu nimecheza kama Starling inaitwa NANI NI HORROR MOVIE wakacheki swagga zangu mule.
Filamu hiyo pia itajumuishwa kwenye EUROPEAN FILM days September-October pale NEW WORLD CINEMA.
Nataka kufanya kazi kimataifa zaidi hapa Music kule Movies lol"

No comments: