22.11.13

Wednesday, July 14, 2010

IJUE MOVIE MPYA INAYOITWA PROMOTA.

Msanii mwenye style kibao ambazo kila akifanya zinamtoa hapa namzungumzia H.Baba baada yakutoa Album yake ambayo inafanya vizuri sokoni inayoitwa GOMA LA USWAZI, sasa jamaa amejikita upande wa pili wa sarafu nikimaanisha upande wa filamu.
H.Baba akishirikiana na Yusuph Mlela waliamua kufunga mabegi yao na kuelekea Tanga kuicheza hiyo filamu iliyobeba jina la Promota kwa lengo lakupata location nzuri huko.
H.Baba akiongea na Bongo Star link amesema filamu hiyo imekamilika na itakuwa inazungumzia tabu za muziki wanazozipata wasanii wetu hapa bongo pamoja na wale mapromota wasio na malengo mazuri kwa wasanii.

Mimi sina la kuendelea ila ndugu yangu H.baba tafadhani naomba copy yangu tu nione kweli mlichokicheza humo ndani kipo mzuka.

No comments: