22.11.13

Friday, July 16, 2010

UKWELI ULIOFICHIKA KUHUSU WIMBO WA NITAFANYA WA KIDUM FT LADY JAYDEE.

Usiku huu nilipokea mail kutoka kwa Producer Hermy B inayosema hivi:
Ngoja nitoe ukweli wa huu wimbo. Kidum alipokuja Dar aliamua kumtafuta Hermy B ambae alikutana nae Project FAME kule Nairobi.

Wakakutana na kufanya kazi pamoja..katika maana ya kwamba mziki huu uliundwa na Hermy na Kidumu akitoa melodies. Drum Patern Yote ni Ya hermy. Kidum aliporudi kule Nairobi akakutana na Rkay(jamaa anaetengeneza mziki wa Wahu examples Sweetlove, Runin Low) madhumuni ni kutengeneza video ya wimbo huu.

Cha ajabu Rkay akamtengeneza Kidum mpaka akakubali kurekodi upyaa wimbo huo. Rkay alikopi kila kitu ila akabadili sauti tofauti kidooogo, ila kisheria alibeba Idea ya kisanii ya Hermy kama ilivo. yote haya yalifanyika bila kuomba ruhusa wala kumpa taarifa Hermy.

Muda ulipofika Hermy alitoa huo mziki kwa radio stesheni, na kidumu alikimbilia kuomba wasiucheze huo wasubiri ule wa Rkay..alipoulizwa huu una tatizo lipi alishindwa kujieleza na akagundulika hana mantiki zaidi ya Ubaguzi wa sanaa tu. Stesheni flani flani wakakubali kuupokea na kuucheza huu wa kwetu Tanzania. Hermy hakutaka kuongea chochote kile mpaka alipoona wimbo huo wa Rkay ukichezwa na upo kwa video aliyopiga Rkay kwa sasa.

Mwenye maskio na aliyeskia wimbo huu mara ya kwanza atajua tu huu uliopo kwenye video ni tofauti na vyombo vimepunguzwa, sio kwamba Rkay hajui kutengeneza muziki, ila alikua akijaribu kujitofautisha sana na Hermy na amejikuta akiharibu kiasi flani sanaa hiyo.

Ninachoomba ni kwamba watanzania tuendelee kushikamana na kupeana suport kwenye wizi wa sanaa kama huu. Tuwe na cha kujivunia kwa watengeneza mziki wetu.
Asalaamu!

8 comments:

Anonymous said...

WIZI MTUPUUUUUU...kazi ya kibongo itasimama milele na milele.,

Anonymous said...

Watu wengine bwana wanasubiri mpaka watafuniwe ndio wameze, thanx Hermy kwa kutujulisha

Jane

Anonymous said...

Ha ha ha ha nimeipenda hii

Musa from UK said...

Tunakoenda mziki wetu unatakiwa maproducer kama nyie mgundue vitu kama hivi, sio ukisikia producer kasample eti kwavile anakaa nje ya bongo ndio ulewe sifa, kama vipi hermy hebu chukua hatua bwana za kimziki kama haki zote unazo

Anonymous said...

KAMA JAMAA ALILIPIA NA KILA KITU ILIKUWA WAZO LAKE HAMY AKAPIGA TU SAWA LAKINI KWA HILI ALILOSEMA HAMY HUO NI WIZI NA HII NI IWE FUNDISHO KWA WEZI WETU WAJUE WA TZ SI WAMESINZIA KAMA WANAVYOZANI NA NDIYO MAANA TUNAWAKOMBA DADA ZAO KIBAO TUNAO HAPA UJANJA HAWANA, MUZIKI BONGO UKO JUU NI NA WATU WANAVIPAJI ILA TU RADIO NA TV ZIMEWAPA KIPAO MBELE HAWA WEZI WA NCHI ZA JIRANI KAMA KENYA NA UG SASA WA TZ TUAMKE NA HAMY PELEKA HUYO R KEY SIJUI ALITAKA KUIBA NA JINA LA R KELLY.

Unknown said...

sasa hermy si achukua hatua....au ndio yale mambo ya kitanzania ya ''HEWALA TU'' huku mtu mwingine anatusua tu na kula bata kwa jasho la mwingine....CHUKUA HATUA MZEE SIO UKAE KIMYA TU...

Anonymous said...

HUU WIZI WA SANAA NI MPAKA LINI JAMANII...KUMBE HUO WIMBO NI WA HERMY B? MI NLIJUA NI WA KENYA HUKO.WATU WEEZI BWANAAA.NYOOO HAMTUWEZI WAKENYA, KAZA BUTI MDOGO WETYU

Anonymous said...

Wadau hapo mi naona Hermy B hajajieleza vizur, Huo wimbo ni wa nani hasa?, na huyo Kidumu yupo chini ya Hermy B ama?.. kama kaamua kuubadilisha ni yeye coz kama Hermy B alilipwa kwa aliyoyafanya haina haja ya kulalamika.. Hayo ni maamuz tu miziki mingap huwa inaingizwa mikono tofauti?.. kama hajalipwa ama na yeye ni mmiliki wa hiyo nyimbo sawa zaid ya yote ajieleze vizur

Mdau