22.11.13

Thursday, July 22, 2010

WASANII WOTE MNAOTAKA KUPIGA HATUA, HEBU MSIKILIZENI JUMA KUTOKA SOUTH AFRICA.

Mambo Mkubwa,
Naitwa Juma Chillemba naishi Johannesburg,South Africa ni mpenzi sana wa Bongo Fleva, Bongo Movies na muziki wa dansi wa kibongo, nyimbo hizi zimekuwa hazionyeshwi kwa wingi katika tv channels za Mnet kama vile Chanel O n.k ukilinganisha na nchi zingine.

Nikaamua kwenda makao makuu yao kuona kulikoni? baada ya kuongea na wahusika wa Channel O pamoja na Africa Magic imedhihirika kwamba miziki na movies zetu zinahitajika sana isipokuwa hawazipati kirahisi kama wanavyopata zingine, hivyo basi najitolea kwa moyo mmoja kukusanya music videos pamoja na movie za kibongo ili nizipeleke kwa mkono kwa wahusika zikaguliwe na kurushwa hewani.

Huduma hii ntaifanya bure ili nijaribu kuwainua wasanii wakibongo wajulikane kimataifa pamoja na kuitangaza TZ kwa ujumla, naomba ujumbe huu uwafikishie walengwa, watakaokuwa tayari wawasiliane nami kupitia facebook,
Email: chillembajuma@yahoo.com au namba ya simu ifuatayo
+27736956002.

Wako Mpenda maendeleo ya wasanii wa kibongo.

Juma Chillemba.

No comments: