TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
USHIRIKI WA WASANII WASIOSAJILIWA KWENYE TUNZO NA MATUKIO YA SANAA NCHINI
Baada ya BASATA kusimamia na kuratibu uanzishwaji wa Mashirikisho manne ya Sanaa nchini ambayo ni Shirikisho la Sanaa Jongevu (Filamu), Shirikisho la Muziki Tanzania, Shirikisho la Sanaa za Maonyesho na Shirikisho la Sanaa za Ufundi kwa lengo la kuvipa nguvu vyama vya wasanii na kuvipa umoja kitaifa,Baraza linapeleka nguvu kwenye urasimishaji wa sekta ya sanaa ikiwa ni pamoja na wadau wote wanaojihusisha na sekta hiyo hususan wasanii.
Kwa mujibu wa Sheria na. 23 ya Bunge ya mwaka 1984, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepewa jukumu la kutambua na kusajili wadau wa Sanaa, kumbi zote za burudani Tanzania Bara na wasanii wote ikiwa ni pamoja na kutoa vibali vya kufanya shughuli za Sanaa.
Lengo ni kuzifanya shughuli za sanaa kufanyika katika mazingira rasmi na ya kufuata sheria za nchi pia kuwatambua wasanii wote nchini kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi yetu.Ikumbukwe kwamba, kufanya shughuli za sanaa bila kusajiliwa na kupewa kibali na BASATA ni kuvunja sheria za nchi na hivyo kustahili adhabu.
Faida za kurasimisha sekta ya sanaa hususan kwa wasanii
1. Kuendesha shughuli za sanaa kwa mujibu wa Sheria za nchi ili kuepuka usumbufu.
2. Kutambulika kwa shughuli ya msanii binafsi, kikundi, Chama nk. hivyo kufanya kazi kihalali.
3. BASATA kama shahidi wa Jamhuri hutoa utambulisho/uthibitisho kwa msanii, kikundi au chama halali mahali popote panapohitajika kwa mfano wakati wa kufungua akaunti benki, kupata VISA, pasi ya kusafiria, mikopo kwenye asasi za fedha, msaada au ushahidi mahakamani.
4. Ikihitajika kuweka ulinzi wa kisheria wa kazi za sanaa,kwa mfano wa Hakimiliki na Hakishiriki.
5. Kuingilia kati pale makubaliano/mikataba ya msanii, kikundi, chama nk. inapokiukwa na kuripotiwa katika Baraza.
6. Kushauri na kutoa mafunzo ya sanaa.
7. Kutafutiwa masoko na/au kuunganishwa na masoko, wasanii na fursa mbalimbali zinapojitokeza.
BASATA linawaagiza waandaaji wa matukio ya sanaa nchini (Tunzo za Sanaa/matamasha/maonyesho) kuhakikisha wanafanya kazi na wasanii waliosajiliwa tu na inapotokea kufanya vinginevyo basi muandaaji wa tukio husika na msanii atawajibika moja kwa moja.
BASATA linatoa hadi tarehe 31 Oktoba, 2010 kwa wasanii na wadau wote nchini kujisajili vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwazuia wasanii pia wadau wasiosajiliwa kushiriki tunzo/matamasha/Matukio ya Sanaa.
Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI, BASATA.

1 comment:
sidhani kama maamuzi haya yalifikiliwa kiundani zaidi na kuangalia athali zake, coz nayafananisha na maamuzi yaliyowahi kutolewaga na waziri fulani wa elimu hapa tz ya kufuta michezo mashuleni bila ya kufikilia kiundani mwisho wa siku ilionekana anauwa michezo kiujumla
sidhani kama ni wakati muafaka wa kuchukua uamuzi huu kwa sasa coz ni asilimia ndogo sana ya watanzania wanaojua ni wapi pa kwenda kujisajili,ni akina nani wanahusika kusajili,ni utaratibu gani unaotumika kujisajili na pia kama kunamalipo ni kiasi gani isije mwisho wasiku ikaonekana wasanii woote wachanga wakajikuta wanaingia ktk kuachana na kazi za sanaa ambako kunatokana na wingi wa ulasimu ktk sekta nzima ya sanaa
kwa maoni yangu mimi nafikili uamuzi mliochukua ni sahii isipokuwa imechukua uamuzi sahihi lakini katika kipindi ambacho sio sahihi kwa tanzania sanaa bado sana tukonyuma tukijinganisha na wenzetu NI HAYO
Post a Comment