22.11.13

Thursday, September 16, 2010

PRODUCER KID BWAY APIGWA NA KUPOTEZA FAHAMU.

Kama nusu saa iliyopita kupitia Clouds FM kwenye kipindi cha XXL mtu mzima Ruben alikuwa anaongea na G Sengo mtangazaji kutoka Clouds FM ya Mwanza na kuripoti taarifa ya Producer Kid Bway kutoka Tetemesha Rec kwamba jana usiku alipigwa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni msanii.
Mtu huyu alikaribishwa studio vizuri na hatimaye baada ya muda mfupi Kid Bway alipigwa na huyo mtu na hatimia kupoteza fahamu na kukimbizwa hospital ya BUGANDO.
Inasemekana Kid Bway alitoka damu nyingi sehemu za Masikioni na puani, na inasemekana hakuna kitu kilichopotea ndani ya studio.

MUNGU AKUPE NGUVU NDUGU YANGU URUDI KWENYE HALI YAKO KAMA ZAMANI.

No comments: