22.11.13

Tuesday, November 29, 2011

VUGUVUGU LA ANTI VIRUS NA HOFU KUBWA YA MAFISADI WA SANAA TZ-WARAKA WA 1


Salaam nyingi kweni nyi wote wapenzi wa muziki hapa Bongo,leo kamanda wenu Mac Temba aka mwanaharakati wa Anti virus nataka kuwapa tafsiri na kuweka mambo sawa yote kuhusiana na mambo kibao yanayopindishwa na kuficha ukweli wa Vuguvugu la kudai haki sawa na uwanja huru wa kufanya sanaa hapa Bongo,kwa jina la mtaani limepewa jina la “Anti virus”

Anti virus ni mkusanyiko wa watu mbalimbali wenye taaluma mbalimbali na uwezo mbalimbali ambao tunaamini kuwa sanaa hii ya muziki inaweza kuwasaidia vijana wengi hapa bongo na pia kuisaidia nchi yetu kupata kodi ambayo itasaidia kuleta maendeleo na kuisogeza nchi yetu mbele kama wenzetu Afrika kusini,Nigeria.Kamwe huu si mgomvi na mtu mmoja wala chombo kimoja cha habari.

Kinachodaiwa hapa ni haki na usawa katika sanaa na malipo sahihi kama wanavyolipwa wakenya na wanaigeria wakija hapa kufanya maonyesho mafupi ya muda wa saaa moja na kuchota mamilioni mengi toka kwa makampuni ambayo yanapata faida toka kwa watanzania hawa ambao wasanii wao wa ndani wanaishi maisha mabovu sana na wala hawakumbukwi na makampuni haya ya bidhaa ambayo hupata mamilioni ya faida toka wa watanzania hawa.

Sanaa  na soka ni fursa pekee ya kumfanya mtoto toka katika familia masikini kuweza kuwa milionea ama kufanikiwa kujinyanyua toka katika maisha mabovu mpaka maisha bora,ni kama mpira ulivyo katika nchi ya Brazil,soma historia za wanasoka kama wakina Ronaldo de Lima na wekina Pelle soka ndilo lililowafanya waweze kujiinua na kuweza kuzisaidia familia zao kupata mafanikio na kuishi maisha bora nay a kifahari.

Hakika naomba niweke sawa hapa Anti virus movement ya kudai haki si ugomvi kati ya Sugu na Ruge bali ni vuguvugu la wasanii wa zamani wanaamini kuwa game ya muziki haiendi sawa na kutaka mambo yawe wazi na BASATA na COSOTA kuundwa upya ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi na kupunguza haya malalamiko na pia watu hao wanaoitwa mapebari katika muziki(hao Virusi katika muziki wanaotafuna mamilioni ya wasanii wetu wachanga wakome),hii ndio sababu ya anti virus na hakika kadiri muda unavyozidi kwenda nashukuru watanzania wanazidi kutuelewa.
Sugu ndiye msanii pekee anayeweza kusimama mbele na kujiita Legendary katika muziki huu  na si mwingine yeyote maana wengi wao ni kama “fisi maji” mnaotaka mabadiliko lakini hamtaki kuongea eti “mtanyimwa airtime redioni” acheni ujinga na kujifanya wanaharakati wakati mnaendelea kunyonywa na mnaishi maisha mabovu wakati sanaa yenu ni kubwa sana na ndiyo kazi pekee inayowafanya muishi mjini,maana wengi wenu mliacha shule kukimbilia katika sanaa cha kushangaza mnaogopa kusimama na kutetea haki zenu za msingi.

Mapambano dhidi ya vuguvugu la kupinga unyonyaji huu hayajaanza jana wala juzi,Solo Thang mwana hiphop anayeishi na kufanya kazi Ireland aliwahi kuingia katika beef na redio moja hapa kwa kudai haki na kuwachana kuwa wanaiba haki za wasanii,wakampiga vita na kumtengenezea kila hila ili kumpoteza,hata wasanii ukiongea nao wanajua haya ila eti wanamuogopa huyo virus eti atawapoteza na kuwanyima airtime ila wako tayari kuendelea kusafriki mikoa yote kwa show ya laki 4 wakati wanaingiza mamilioni ya shilingi.

Inashangaza eti msanii kama Lina eti anaambiwa ana mafanikio kwa kuweza kununua gari aina ya “Vitz” baada ya kuuza albamu na kufanya show kibao,je haya ni mafinikio kweli kwa mauzo ya albamu Bongo?haya ndio mambo tunayopigia makelele maana zamani adui wa wasanii alikuwa mdosi lakini siku hizi mpaka huyo Virus sasa ndiye anayeamua kusambaza albamu za wasanii wetu na nani apewe shilingi ngapi kwa albamu yake.

Ni wasanii wangapi wa hapa kwetu wenye kuishi maisha ya kueleweka na kumiliki vitega uchumi na kuweza kuendesha maisha yao???hakika hawazidi kumi kwasababu wengi wanapambwa redioni lakini ki uhalisia hawana cha maana,hebu ona wsanii  kama Mr Nice,Bushoke,Gangwe Mobb,Feroos,East Coast Team walivyotumiwa na alivyotupwa na hao wadau,Sio kwamba wametumia pesa vibaya bali asilimia kubwa ya pesa hizo huliwa na hao wadau na kuahidiwa eti promotion ya albamu ijayo.

Hili si sawa ndio maana katika hili tunataka wanaojibu hoja za Anti virus wajibu hoja na sio propaganda za kitoto maana watu wameamka na wanataka majibu na uwanja huru katika sanaa,kila mwenye fursa na uwezo katika sanaa afanye bila kubughuziwa,sanaa iwe huru na vyombo vinavyosimamia sanaa viweze kufanya kazi bila mikono ya hawa virus aka mabepari wa sanaa wanaopigwa vita.Huu sio ugomvi wa watu wawili hapana,haya ni mapambano ya kudai haki na usawa katika sanaa yetu maana sanaa si ya watu wachache.

Kama mambo haya ya sanaa yetu yangeweza kuwa wazi na fair tungeweza kuwa na wasanii wenye mafanikio kama lady Jaydee wengi sana na hakika wangeweza kuwavutia mabinti wengi kuingia katika sanaa hii lakini ukimtoa lady jaydee taja mwanamuziki mwingine mwenye mafanikio kama yeye,Kuna siku moja niliona mahojiano na msanii mmoja mkubwa wa hip hop bongo anayejiita legendary akisema mafanikio yake katika gemu toka aanze miaka zaidi ya kumi nyuma ni nyumba na gari Spacio!!! Daah inasikitisha sana unapoona msanii kama Nonini wa juzi juzi sasa hivi ana mafikio makubwa na hafanyi show chini ya dola 2500 na ukiwataka P unit ni dola 3000  lakini katika show hiyohiyo msanii wa bongo analipwa laki 4 na wengine mpaka bure kwa ahadi ya kupewa airtime redioni kwao,huu ndio wizi tunaousema uishe maana ni lini msanii wetu atakuwa na mafanikio kama malipo ndio haya.

Hofu kubwa ya kundi hilo la mafisadi wa sanaa hapa Bongo ni kuwa haya mambo yakiwa wazi watakosa pa kuiba na kufisadi ndio maana wanapandikiza mamluki na kujibu majibu ya ki propaganda na kukimbia hoja za msingi,jambo moja ambalo wanapaswa kulijua ni kuwa hakuna jambo ambalo halina ncha.

katika hili muda umefika,jana kwenye facebook mambo mengi yamejiri na comments kibao mmoja wa wadau wa muziki Pkay alindika “the fall of Roma empire…wake up kids…maji yakizuiwa njia hutafuta mkondo mwingine,someni alama za nyakati”

Dada Maria Sarungi- Tsehai yeye aliubatiza huu mwamko kama Sugu phenomenon katika ukurasa wake wa facebook jana na kusema “Angry young men ambao wamechoka na wameamua kujiexpress kupitia muziki,ni hatua nzuri ila isiishie hapo…”

Carren Flora Mgonja kwenye wall yake ameeandika”Asanteni vinega kwa kutupa show tukioikosa kwa long tyme,I salute my brothers,safi sana Adili na songi lako peke yangu,Soggy na kibanda cha simu”

Hili mimi nililijua litafika hapa maana hakika ni jambo ambalo tulikiwa tunalizungumzia mara kwa mara katika mijadala na wadau wa muziki huu kuwa kuna watu wachache wanaohodhi mamlaka na kufanya mambo katika sanaa yasisogee mbele kwa manufaa yao binafsi,napinga sana suala hili “eti muziki wetu haulipi”nani kasema muziki haulipi?mbona hao wadau ni muziki huu huu umewafanya mpaka wameweza kufungua TV,muziki huu huu ndio unaowafanya wao kununua magari ya kifahari.

Nguvu ya mabadiliko ya watu haipingwi kwa vijembe redioni wala maneno ya shombo,bali kwa Hoja zenye msingi na zenye majibu na si kwa hoja nyepesi jamani,wasanii wengi wamejazwa fikra kuwa huu ni ugomvi binafsi kati ya watu wawili,hakika sio kweli,suala la Malaria No more limepita sasa tunasonga mbele na kutaka kila msanii kweli apate kipande chake halali na kuacha kutengenezewa wasanii na kikundi kimoja cha watu kwa maslahi yao.Miaka miwili iliyopita walianzisha mizengwe eti Hip Hop hailipi na kuwavuruga sana wasanii na wale wachache wasioweza kupambana wakaamua kuanza kubana pua ili wapewe airtime.

Kwa muda mrefu nimekuwa mdau na naufahamu muziki huu kwa upeo mkubwa sana na ndio maana nayaongea haya bila woga,ifike muda kila mtu akafanya jambo analolijua na sio kubahatisha,kuna  jamaa mmoja eti ni “music director “wa redio moja hivi ya fm hapa mjini  eti yeye kazi yake ni kusikiliza nyimbo na kutoa kasoro na marekebisho cha kushangaza huyo anayeitwa music director hana hata diploma ya muziki huo,unawezaje kukosoa kitu amabcho hukijui na kutenda haki???haya ndio mambo ya kimagumashi yanayoharibu muziki wetu,get a life boy na kama unataka kufanya mambo nenda shule japo diploma itakupa msingi wa kufanya hayo.

Miaka michache iliyopita alivuma msanii Mb Doggy na kutajwa kuwa ameuza kopi zaidi ya laki moja katika siku mbili za mauzo ya albamu yake ya “Lafifa”daah akapewa coverage kubwa na mengi yakasemwa ooh kavunja rekodi mpaka kawafunika jamaa wa bendi lakini hebu mtafute Mb Doggy leo kaa nae umuulize uhalisia wa yaliyotokea,utasikitika na kuduwaa,leo hii Mb Doggy anapambana kurudi upya kwenye game japo apate hela ya kuishi,hii ni hatari sana.

Wasanii wa bongo amkeni acheni kufanywa misukule na kutumiwa kama daraja la kupata mafanikio ya watu wachache na aminini kuwa hata nyie mnauwezo wa kufanya makubwa na kumiliki magari ya kifahari kama chameleon,Nonini,Bebe Cool ama Nameless na kuacha kuishi maisha ya kuunga unga wakati you got all the means to be on Top,Bila kuamka na kupigania hili hakika mtazeeka na kukosa la kuwaelezea watoto na wajukuu,Hata marehemu mzee Kipara wa kaole alikuwa kijana kama nyie hebu ona maisha ambayo alikuwa anaishi mpaka mauti ikamfikia.inasikitisha na bila kutumia ujana wenu sahihi hakika mtakuwa mizigo huko uzeeni.

Waraka wa pili utakujia tena jumatatu ijayo>>>>hii ni kwa ajili ya wapenda muziki wote na kupata ufahamu ya kinachoendelea kwenye Anti Virus Movement ya kuokoa muziki huu wa Bongo usiendelee kupotea na kufaidisha kundi dogo la mabepari aka Virusi.
  
ALUTA CONTINUA….
Anti Virus Activist -MAC

24 comments:

Anonymous said...

HAKUNA MTU ALIAMINI KAMA CKU MOJA USSSR ISINGEKUAPO KATIKA DUNIA HII...KAZENI WANA EVERYTHING KINAWEZEZEKAN

Anonymous said...

NA PIA UNAKUMBUKA HAWA WA@&NGE WALIVYOKUA WANATENGENEZA BEEF LA DUDUBAYA NA MR NICE..AT ZE END WASANII WOTE WAWILI WAKO HOI KIMAISHA BY ZE TYM WAO WANAWAUA DADA ZETU KWA NGOMA KWA KUAWAHONGA MAGARI YA MITUMBA

leah said...

nimeupenda walaka na najua mlipofikia ni pa zuri, mimi si msanii, ila ninajua kiasi chake haya mambo, wakati nasoma walaka huu kuna jambo nimelifikiria na nahisi linaweza likawapeleka sehemu nyingine zaidi, umeelezea jinsi wasanii kama mb doggy walivyopotezwa na kuwa na maisha mabaya amabyo hayalingani na maslahi wanayotakiwa kupata

nililolifikiria ni kwamba, mngeweza kutengeneza documentary fupi,ya video, mkawachukua watu kama hao wakina mb dogy waeleze ukweli wanaoujua hadi wao kufikishwa hapo walipo, kisha mkatafuta air time katika chombo cha televission chochote mkakirusha hewani, nina uhakika watu wakiona kwa macho yao jinsi msanii mwenyewe anavyohadithia itawabamba wengi na hawatakuwa na pakutokea, mnaweza fanya like a season, wiki hii mbdogg akaongea yake, next time mwingine , next ivyo ivyo, ninauhakika mtasacceed, angalizo ni kwamba tumieni rugha kali lakini zinazoongeleka i mean si matusi, onyesheni ustaarabu ili isionekane ni beef ila ionekane kama ni wanaharakati

like this hope mtasucceed
ciao

Anonymous said...

thas good Sugu tatizo la wasanii wa Bongo hawajiamini na zaidi hawana uhakika na wanacho kifanya..Bado wanahisi mziki kwao sio kazi ndo maana wanadhulumiwa na kuburuzwa kama watumwa wasioweza kujitetea..Amkeni wasanii wa Tanzania mda wa mabadiliko umewadia piganieni haki zenu lasivyo mtaishia kupiga deki nyumbani kwa watangazaji...i like ANTI VIRUS..

Anonymous said...

uvivu tu haki miliki hakuna mnataka mlipwe kama p did hii si aibu jamani fanyeni kazi kupandisha muziki wenu uvivu huu jamani utawapeleka pabaya ona mtu kama AY juhudi yake na anafanya kazi nyingi nje nyie hamjiendelezi kimziki hamko profenal kabisa hamna manegers hata hao wenye mameneja na hao mameneja hawajui kitu halafu mnapiga kelele tutaendelea kununua kazi zenu ubungo sijui mtasema nani anawanyonya ni ushamba na umbumbu wenu mimi binafsi kazi za wasanii ambazo naweza nunua hazizidi watano zingine zote utumbo hamna kitu mnafanya albamu nyimbo 15 nzuri mbili tutaishia kubani tu vibandani

Anonymous said...

b

Jayla@kenny said...

Now i get more knowledge abt antivirus...thank u @dj choka

Anonymous said...

Kweli tupu na hao wasanii wengine wanaojiita wanaharakati kwa maneno wakati wanashindwa kuonyesha ukongwe wao wa fikra wabadilike kweli wanaboa big up sana mwandishi wa makala hayo

£rick $hubby said...

vinega mwanza pia tunaunga mkono,naomba tufanye mambo wazi kama vip tuwaanike wazi nawasio naupeo wa haya wawajue.vitus buyamba & Shuby Gnstr

Anonymous said...

PELEKA JAMII FORUMS. KUNA MPUMBAVU KULE ANAITWA "NYANI NGABU". YAANI NI NYANI KWELI KWELI. KAMA NI KIRUSI YEYE NI NYANINGABULIASIS

Anonymous said...

Dada leah ushauri wako mzuri sana lakini tatizo hawa wanyonyaji wametumia trick moja - wamefanya suala liwe la kisiasa. Kwa hiyo Sugu ingawa ni mwana harakati na vile vile mwanasiana anachukuliwa kama ni Chadema na kwa hiyo anapambana na CCM! Unaona sasa mambo yalipoharibika? Jambo la wazi la haki ambayo wafaidi wote bila kujali vyama vyao limefanywa siasa makusudi ili lisishughulikiwe ipasavyo. Surprisingly, wafuasi wa pande zote zi kama ni wanasiasa as such, wanatafuta maslahi tu lakini wakubwa wamefanya suala liwe la kisiasa!

Anonymous said...

WOTE NI WAJINGA NA WAFUPI WA FIKIRA! UNAJUA WASANII WENGI HUWA WANAJISAHAU SANA WANAPOPATA MAFANIKIO. UJUA ANGALIA MWANAMUZIKI FERUZI ALIKUWA NA PESA SANA ILA LEO ZIPO WAPI??? SI AMEFULIA KWA UJINGA WAKE MAANA HAKUWA NA MALENGO, GARI ALIUZA NA MPK LEO ANAISHIA KUPANGA MAISHA YAMEKWENDA KOMBO. MAISHA NI MALENGO KWA KILE UNACHOKUWA UNAKIPATA NA KUIFANYIA KAZI. WASANII INUKENI ACHENI KULIA LIA NA KUSINGIZIA WATU WANAWAANGUSHA. TATIZO MNAJIANGUSHA WENYEWEEEEE. FUNGUKENI FANYENI VITU VYA MAENDELEO UNAPOPATA HELA JARIBU KUJIPANGA KIMAISHA MUZIKI WA TANZANIA NI KAMA PIPI UKILA UTAMU UNAISHA KESHO HAUDHAMINIKI TENA.

Anonymous said...

aliye na macho ataona na aliye na masikio asikie.Gud looking SUGU, pamojah!!!

frank said...

nimeipenda hii...tatizo la wasanii wetu wa bongo ni umaskini na woga wa mabadiliko....naungana na mmoja wa wachangiaji tafadhali tengenezeni documentary itakayoelezea haya yote i think itaongeza uwelewa kwa watu

Anonymous said...

hii movement isiishie dar please fanyeni tour tz nzima ili kusambaza uelewa huu

Anonymous said...

Big up sana mzazi kumbe nawe ni mdau..wa antvirus fanya kweli c hiyo pia zipo nyingi katika youtube jaribu kuzitupia hapo kati mixtape ya antvirus volume 2 na nyinginezo jaribu kufikisha ujumbe ufike kwa style hii mafanikio ya mziki yatasomeka tu hata kwa ma DJ c kwa kubadilisha masupra tunahitaji kuona wamdau wakubwa kuona munamiliki majumba na gari ya kifahari tunahiji mapinduzi ya kweli mzazi...nasomeka kama Duller Azaram on facebook mdau no.1 wa antvirus Mtwizi

Anonymous said...

Nahisi sasa nime elimika na hili swala la ANTI VIRUS. Dhamira ni nzuri maana wahenga wamesema "Kimfaacho mtu chake". Ushauli wangu ni kuwa mtumie lugha Inayokubalika na wengi yenye staha(siyo matusi).
Kuna mdau hapo juu ameongelea swala "mngeweza kutengeneza documentary fupi ya video" hiyo ni idea nzuri tena sana nahisi itaeleza jamii nini kinachotokea. All da best in this, Inshaalah kheri.

Anonymous said...

NARUDIA TENA KUSEMA; MAISHA NI MALENGO KWA KILE UNACHOKUWA UNAKIPATA NA KUIFANYIA KAZI. WASANII INUKENI ACHENI KULIA LIA NA KUSINGIZIA WATU WANAWAANGUSHA. TATIZO MNAJIANGUSHA WENYEWEEEEE. FUNGUKENI FANYENI VITU VYA MAENDELEO UNAPOPATA HELA JARIBU KUJIPANGA KIMAISHA MUZIKI WA TANZANIA NI KAMA PIPI UKILA UTAMU UNAISHA KESHO HAUDHAMINIKI TENA.

Anonymous said...

Embu angalieni jinsi vijana wetu wanavyo ishia kula unga kwa ajili ya frustration. Jina kubwa mfukoni hata jiti kukaa siku mbili ni tabu. Naanza na list ya unga

Banza
Msafiri diof, Awa ivi twanga ime wapa nini adi leo.
Ngwair- teja zuri tu.
Daz baba- hayaaaa
TID- teja la siku nyingi tena Luge ndo kampoteza uyu jamaa.
List ni ndefu aisee.

Haya na waliokuwa wana harakati sugu kipindi cha 2005
Kalapina na kikosi cha mizinga sasaivi wame give up na wapo na mawingu mtindo mmoja. Shauri ya msoto wa maisha na sio kwamba wanapenda.

KWELI FANYENI HIYO DOCUMENTARY NA HAO WOTE MUWATUPIE. OKOENI HILI TAIFA LETU.

Anonymous said...

Big up kwa hii movement, mwanzo ni mguu,lakini ikishaeleweka hata hao wanao wapinga watakula matunda haya, haingii akilini kabisa msanii kama yule pablo snoop achukue mahela kibao kuja kupiga show hapa,kisha mtu kama niki mbishi avute kidogo, hii ni movement inabidi wasanii wote waungane ni juu yao, watu wanachakachia mahela kibao mifukoni, wake up my brothers and sisters ni kwa ajili yenu wote hii, stand together, na ikitoka hapa ihamie kwenye mpira, ni lazima mambo yabadilike, vilabu vya mpira vinavute kama mil 800 kutoka fifa kila mwaka, watu tunajuwa sema ndiyo hivyo hata kulalamika utamlalamikia nani, lakini kukiwa na movement kama hizi mnakuwa pamoja bwana, DJCHOKA wewe ni nguvu kazi bwana na Mgambo haswa, kuna wengine hata kuweka kama ilivyo wanaogopa ni watumwa wa kifrikra tu, halafu hapa kuna mtu kacomment sijui AY mbona anatoka, Embu niambia juhudi anazofanya AY kutoka kama mambo yangekuwa sahihi hapa bongo angekuwa zaidi ya alivyo, usidanganyike na mafanikio kiduchu tu aliyonayo, ata yeye anatakiwa ajoin kwenye hii movement,fa,diamond, sijui nani na nani wooote yani wajoin, embu angalia wale twanga waliopelekwa uk, hela yote anapiga yule dada wakati kazi wanafanya wao, lazima kila kitu kilipe bana. BIG UP ANTI VIRUS MOVEMENT kitaeleweka tu.

Anonymous said...

hakuna lolote wasanii wa bongo wanajiangusha wenyewe tusidanganyane bureeeeeeeeeeee

Anonymous said...

HONGERENI KWA MOVEMENT ILA MI NAZANI PIA WASANII WETU HAWANA MISIMAMONA WANACOKITAKA IVI KAMAMSANII UKIJIWEKEA DAU LA WEWE KUPAFOM NA KAMA MTU HANA IYO PESA HUPIGI SHOO YAKE UNAZANI MWISHO WA SIKU ITA KUAJE?SI LAZIMA WATAKUBALIANA NA UNACHO TAKA?NA PIA WASANII WETU WAKITAKA KULIPWA VIZURI LAZIMA NA WAO WAFANYE VITU VIZURI VINAVYO KUBALIKA NA JAMII,MPAKA SSA NAONA WANAOFANYA VIZURI WANAHATA MAJENGO SASA MFANO WAKINA DIAMOND,JMO,MADII WENGINE WENGI,KIKUBWA HAPA NAOMBA WASANII WAWE NA MSIMAMO WEKA DAU LAKO KAMILI USIYUMBISHWE NA PESA NJAA NI BORA USPIGE SHO KULIKO KULIPWA ELA AMBAYO UNAONA HAINA MASILHAI KWAKO.

Anonymous said...

Nimesoma wakala uko poa na kweli tupu wadau wengi huko juu mmechangia poa sana sema kuna kidudu mtu amekosea kusema wasaniii wenyewe hawajipangi,,unajua swala hili si la kuliongelea kama hujui its better ukanyamaza na kusoma tu watu wanayoyaandika,,mi najua mengi sana nimeshafanya kazi na wasanii kupitia gazeti flani hapa town,kiukweli utawaonea huruma wasanii wanaibiwa lakini wanakuambia noma siwezi kuzungumza coz nitabaniwa air time na kufichwa kwa gharama yoyote na hao wadau,,tuwe wakweli guys huu kweli si ugomvi kati ya sugu na Ruge ila niamini mimi Clouds ni VIRUS number moja katika swala la kuwaibia wasanii,,nawapa story kadhaa why nasema hivi ..nimefanya kazi na wasanii takribani 40 ama 50 wa music,wanasema wahindi ambao ni wasambazaji wa kazi za wasanii kuna watu wanawaamini sana wakiambia kitu na hao watu naomba niwaweke wazi baadhi yao Adamu Mchomvu, B12, Gadna G.Habash..so kinachofanyika ni hivi kama utakwenda mwenyewe kwa muhindi anaweza akakuambia nitakugongea copy elfu mbili kama kianzio kucheki upepo kama utauza ama la ila ukipelekwa na hao watu niliowataja hapa juu coz wanaaminika utagongewa copy mpaka elfu 50,,so wizi unakuja wapi sasa kwanza msanii unaambiwa ujaze mafuta ya gari ya hao viumbe, then katika kila copy na yeye ana chake ni kati ya sh.50 mpaka 200 guys piga mahesabu kama anachukua sh.200 katika kila copy akigongewa copy elfu 50 atachukua kiasi gani?then kesho katika show unajifanya unatetea maslahi ya msanii jamani hivi ni kweli hapo,,Guys Ant Virus wanajua nini wanachokiongea na ni ukweli mtupu trust me niliwalazimisha hao wasanii waongee hili walikataa kata kata wakati wanatuambia huku nyuma ni tabia inayowaumiza sana sema hawana la kufanya,,,meeeeeeen wake up watu kweli hapa mjin wana maisha ya juu kwa kupitia migongo ya wasaniii vibaya mno..nawapa ishu nyingine japo sitaweza kuielezea sana ila ni kwa mawazo tu guys lets be honest kuna wasanii wakali kweli kushinda hao ambao wapo T.H.T lakin coz wao wamegoma kuibiwa hawana unafuuu katika hili game,,mfano mdogo tu sidhani km kutoka T.H.T kuna msanii anayemfikia kwa kiwango Q.Chillah but haonekan coz hataki kuibiwa leo hii eti eti barnaba yuko juuuuuuuuu kumshinda Q.chilllah nooooo I dony buy that...wajamen tuungeni mkono Anti Virus Movement nawaambia itafika siku mtaamini wanachokipigania hawa jamaa Trust me,,ifike tym tuwaconvince watoto wetu wafanye music coz utakuwa unawatoa katika umaskini lakin sio kwa hivi sasa they just have names with empty coin dammmmmmmm.Anti Virus ni MAPAMBANO YA UKWELI TUKO PAMOJA MWANZO MWISHO MAPKA KIELEWEKE..ITS NOT ABOUT SIASA AMINI HILO.

Anonymous said...

Yap kiukwel maisha ya wasanii ni magumu sana kuna siku nilikua kariakoo na nunua mkanda wa kiunon gafla akaja msanii flan akataka kununua kofia alipo ambiwa kofia inauzwa elfu 15 aliomba kupunguziwa bei uku akilalamika kama kwa dakika 25 hivi! Je haya ndo maisha bora kwa msanii wa kitanzania? GUYZ WAKE UP NA TUSEME IMETOSHA SASA!