22.11.13

Wednesday, April 11, 2012

LULU MICHAEL BAADA YAKUFIKISHWA MAHAKAMANI.

Habari hii na BBC Swahili

Msanii wa kike wa filamu Tanzania Elizabeth Michael Kimemeta maarufu kama Lulu,amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwingine wa filamu Marehemu Steven Kanumba.
Amefikishwa mahakamani ikiwa ni siku nne, tangu alipokamatwa mara baada ya kifo cha msanii huyo ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.
Mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam,Bi Augustina Mbando,Elizabeth Michael Kimemeta ajulikanaye kama Lulu kwa jina la Usanii,aliwasili mahakamani hapo akiwa chini ya Ulinzi mkali wa askari Polisi waliokuwa wamevaa kiraia na wengine wakiwa wamejihami kwa silaha.
Mara baada ya Kufikishwa mahakamani,upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa serikali Bi Elizabeth Kaganda ulimsomea shtaka moja ambalo ni la mauaji, kosa ambalo ni kinyume cha sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 196.
Wakili huyo wa serikali Bi Elizabeth Kaganda,alidai mbele ya mahakama kuwa mnamo tarehe 07 mwezi April mwaka 2012,katika eneo la Sinza Vatican,msanii Elizabeth alimuua msanii Steven Kanumba.
Akiwa amevalia gauni kubwa lijulikanalo kama dera lenye rangi ya Njano mtandio wa rangi ya waridi na kandambili nyekundu mshtakiwa alionekana kutokuwa na wasi wasi pamoja uzito wa tuhuma za mauaji anayokabiliwa nayo huku akijibu maswali kadhaa kuhusu wasifu wake.
Msanii huyo alikanusha kuwa na umri wa miaka 18 baada ya kuulizwa ,ambapo yeye amesisitiza kuwa ana umri wa miaka 17, hii ikiwa ni tofauti na habari ambazo zimekuwa zikiripotiwa kuhusu umri wa msanii huyo ambaye sasa anatambulika kama mshtakiwa.
Kesi hii ya mauaji inatajwa kwa mara ya kwanza na mshtakiwa hakutakiwa kukiri wala kukana mashtaka.
Upande wa mashtaka umeieleza mahakama kuwa kesi bado iko kwenye upelelezi ambapo inatarajiwa kutajwa tena April 23 mwaka huu.
Mshtakiwa amepelekwa rumande hadi siku hiyo wakati kesi hii itakapotajwa tena.
Kwa upande mwingine tukio la kufikishwa mahakamani kwa mtuhumiwa huyo kumefanywa kwa usiri mkubwa na kufanya waandishi wa habari wengi wameshindwa kufuatilia kwa karibu tukio lenyewe.
Kufikishwa mahakamani kwa msanii huyo na kusomewa shtaka la mauaji ya Kanumba kumetokea siku moja baada na Marehemu Steven Kanumba kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Mazishi yake yalichukua sura ya kitaifa kutokana na umaarufu aliojijengea msani huyo katika jamii ya watanzania na hata nchi za nje.

13 comments:

Anonymous said...

From report ya so called madaktari bingwa wa muhimbili...info yao ina utata...wanaeleza from the 2 and half hour post mortum they did..wameona kwamba kilicho cause death ni mtikisiko wa ubongo...they insisted it was the cerebrum...well am not that good in biology...but from what i know cerebrum controls memory and thinking...cerebellum (back part) involves balancing and maintainance...then kuna brain stem which maintains human life...and involves breathing, heartbeat, swallowing etc...and it connect to the spinal cord...so design hao madaktari mabingwa wanaeleza info ambayo ina utata...na sio kweli..they said kanumba died from mtikisiko..ambayo ni brain concussion...they aka shindwa kupumia ambayo ndo inatakiwa kuwa brain stem or also called medula had been injured
so sio kwamba mtikisiko wa cerebrum..angepata hiyo angekuwa amepoteza fahamu tu...ni hayo tu. R.i.p kanumba
pass the info djchoka

rajabu893 said...

Jaman huyu bint kimeo wiki 2 zilizopita alihojiwa na salama kweny mkas akasema anamiaka 18, acha na hiyo aliwah kuhojiwa na zamarad kweny tek 1 na video ipo youtube alisema ana 18 na kafanya na birthday. Aaakudanganya watanzania

Anonymous said...

HUYU MTOTO WACHA YAMKUTE KWANI MWANA KUYATAKA SASA KAYAPATA SIJAONA MTOTO BALAA HUYU JAMANIIIIIIIII SIJUI JAMII ITAKAMPOKEAJE AWE AMETENDA AU HAKUTENDA CHA MOTO ATAKIONA KWA JAMII YENYE MAPENZI NA KANUMBA SIJUI ATAPITA NJIA GANI VILI VIDOLE TU ATAKAVYOONYESHWA HATA NA WATOTO WADOGO NDIO VITAVYOMUADHIBU HUTOKUWA NA AMANI KILA UNAPOKATISHA MITAA UNAITWA MUUWAJI

Anonymous said...

ni kweli mchangiaji uliyechangia hapo juu hata km ataachiwa huru na kuonekana hana hatia lakini maisha yake yako hatarini kwa jamii ya kitanzania inayomzunguka sijui mwisho wa huyu mtoto utakuwaje manke mfano mdogo umetokea pale makaburini watu wamemuone m2 km lulu ndani ya gari wakawa wanalifata kwa hasira na maneno kibao si mwezetu huyu lazima tumukumu kwa kutuulia kipenzi chetu kanumba haya ngoja tuone itakuwaje

kenyanbabe said...

Ano1 yaani wat ur saying is true, wengine imebidi tuanze kusoma biology baada ya hili swala tujue ni nini. Hasa,@rajabu hawa waongo sana basi haina haya ya sisi kuwasikiliza kama ni uongo bora wasiende kwenye hizo interviews.

Anonymous said...

Huyo dogo amechanganyikiwa anatakiwa aombewe.

Anonymous said...

kwaiyo uyu binti mwaka huu ndo anatimiza 17???????????kweli mjini kuna kazi ila wacha dunia imfunze mna mama ake halishindwi kumfunza adamu.

Anonymous said...

wadau pitieni blog yangu www.maggietzee.blogspot.com

ni mpya mnipe maoni

Anonymous said...

SI ALIKUWA ANAUTAKA UKUBWA NDUGU YANGU NDIO KAUPATA SASA

Anonymous said...

HUYU BINTI SIO KIMEO TU NI HAKUNAGA KABISA AWAAMBIE WA2 MDOOGO AKOSE WANAUME KM BABA ZAKE HIKI NDIO ALICHOVUNA

Anonymous said...

MAJI YAMESHAMFIKA YA SHINGO ANALIA YEYE NI MDOGO UNACHEZA NA SEGEREA NINIIIIII.......... TUNAJUA UTATOKA ILA NGOJA UPATE ADABU KWANZA LADA UTABADILIKA

Anonymous said...

halafu na huyu mwanaume mwenzetu anaongea nini sasa? nina maanisha baba lulu, mbona anatutia aibu wanaume wenzake, alikuwa wapi katika malezi ya lulu?

Anonymous said...

Huyu demu mi simjui, lakini inavyoonekana watamwachia tu kwasababu ya udhaifu wao. Naona hadi Afande kanogewa kasahau yupo kazini, katolea macho matako, duuuh.