22.11.13

Wednesday, April 11, 2012

TUMEJIFUNZA NINI KATIKA MSIBA WA KANUMBA SISI VIJANA?

Kanumba kazikwa hivyo kwa sababu nyingi sana baadhi ni kwamba

1.Ni mmoja ya msanii ambaye hakuwa na skendo ambazo zilikuwa zinaleta picha mbaya katika jamii na katika Tasnia hiyo ya Filamu na hata pale waaandishi walipotaka kuuza Gazeti aliwakemea huyo ni msanii makini sana
2.Hakuwa mbinafsi kwani tumeshuhudia vijana wengi kawaibua katika Filamu zake mbalimbali
3.Hakuwa na Majivuno Kwa kiwango alichokuwa amefika Kanumba leo angetafuta watu fulani wa kuongea nao lakini hakuwa hivyo
4.Alipenda jamii ndiyo maana aliweza kutoa misaada mbalimbali kwa makundi tofauti na ndiyo maana Jamii imejitokeza katika kumuaga
5.Hakukatishwa na Maneno ya watu wasiopenda mafanikio ya wenzao
6.Aliipenda sana nchi yake kwa dhati na popote alipenda kusema natoka Tanzania
7.Kanumba hakubagua huyu wala yule ndiyo maana kazikwa na watu wengi wa rika tofauti
8.Alikuwa kiongozi kwa wenzake.
9.Alichukia umaskini.
10.Kanumba alijipenda na alipenda kutengeneza Historia hapa Duniani

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo niliyajua kwa Kanumba baada ya kuwa na Mafanikio ya haraka katika tasnia ya Filamu,nilitamani sana kufika katika mazishi lakini sikuweza,aaaaah Kanumba ipo siku nitafika kwenye kaburi lako japo niseme neno ambalo siku zote nilipenda nikwambie lakini sikuweza kukutana nawe na hilo neno ni hili hapa HONGERA KAKA KWA KAZI ZAKO hili neno sijakwambia lakini ipo siku nitakwambia tutakapokutana katika uzima wa Milele

5 comments:

Hamady Bendera said...

He Is dead n' gone!

kenyanbabe said...

So touched can't stop crying ! Hmm

Anonymous said...

Wanaume,acheni ufatataki..kuwala watoto wadogo ni sawa na kubaka..lulu bado ni mtoto,kwa hiyo woote mliompitia mlikuwa mnambaka na kosa hili ni miaka 30 jela

Anonymous said...

surely He will be missed RIP RAFIKI will meet again

Anonymous said...

Wewe Anonymous wa apr 14 kama ulikuwa huna chakuandika bora ungekaa kimya kuliko kutuchafulia hali ya hewa humu ndani,RIP mpendwa wetu Kanumba tutakukumbuka milele adi siku na sisi mungu atakapotuita mbele ya haki.......we still love u sanaa sanaaaa Kanumba,na atujui kama kuna msanii atakayekufikia....!