22.11.13

Tuesday, July 31, 2012

YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA, GOSPEL, DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.

Husika na kichwa cha habari hapo juu, 

Kwa ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agzio kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na Callertunes katika mitandao ya simu ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya kazi. 

Sababu ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.


Sababu ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya pato toka kwenye shoo.

Hivyo tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa njia ya Television , Radio , blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno mpaka hapo tutakapofikia muafaka.


Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.

Mwisho tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.

Asante.

4 comments:

streetvoice said...

SAFIIIIIIII

Anonymous said...

Tuonyeshe saini ya hao waliosaini na majina yao,sio unajitungia vitu utkuja rekebishwa ndio ujue huna sauti wala thamani yoyote katika mziki wa bongo mtoto mdogo wewe kanyonye!

Natasha Shyrose said...

Amka Afrika - Natasha Shyrose
Bora mnaamka vizuri sana wazo hili! Natumaini waimbaji watapata haki zao pia! Bora huko sasa huku wanataka show bure. Bure kafa tunataka vipaji vya mziki kutengeneza tuu mziki wenyewe unabei kubwa sana...
Halafu hao hao akija mwimbaji wa nje wanapewa kila kitu. Natumaini kutakua na mabadiliko. Ili waimbaji na wasanii waendelee kazi zao

Anonymous said...

hawata kosekana wenye tamaa ndogondogo na wasliti so kueni makinai