·
Ushirikiano utawawezesha wateja kukata tiketi
kupitia huduma ya M –pesa.
·
Huduma kurahisisha malipo ya tiketi
Dar es Salaam, 30th
Agosti, 2012 … Kampuni ya usafiri wa anga ya Precision air
hii leo imeingia kwenye mkataba na Vodacom Tanzania ambapo wateja wataweza
kulipia tiketi za usafiri kupitia huduma ya M-Pesa.
Ili
kufanya malipo mteja atatakiwa kupiga namba *150*00# na kuchagua malipo ya bili
kupitia orodha ya M-pesa na kuingiza namba ya biashara ya Precision Air ambayo
ni 333777 ikifuatiwa na namba ya malipo na kiasi cha
fedha itakayolipwa.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha
kampuni ya Precision Air, Patrick Ndekana, amesema kuwa njia hiyo ni ya haraka,
rahisi na itaokoa muda kwa wateja.
“Tunafurahi kuingia katika ushirikiano huu na
Vodacom Tanzania, Tunawahimiza wateja wetu kutumia huduma hii ili kuokoa muda
na kufanya malipo yao katika njia ambayo ni rahisi na ya haraka,” alisema
Ndekana.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Kifedha cha Vodacom Tanzania, Innocent Ephraim, alibainisha
kuwa ushirikiano huo utatoa njia badala katika malipo ya tiketi, na kusisitiza
kuwa huduma ya M- pesa ni salama, haraka na niya uhakika, kwa kuwa imeleta
mapinduzi katika huduma mbalimbali za kifedha tangu kuanzishwa kwake miaka
mimne iliyopita.
“Tunaamini
kuwa tutatoa huduma bora kwa wateja wetu. Tunajivunia ushirikiano huu na
tunatarajia utakuwa na mafanikio makubwa katika kukidhi mahitaji ya huduma kwa
wateja wetu,” alisema Ephraim.
Huduma
ya M-Pesa ya Vodacom Tanzania ina mawakala zaidi ya elfu 20,000 nchini kote, na
ni pekee ambayo inaongoza, kwa usalama na ubora katika kukidhi mahitaji ya
huduma za kifedha kwa Watatanzania walio wengi.
Kampuni
ya Precision Air inatoa huduma zake katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, na
kufika katika maeneo mengi ya nchi kwa siku.
Sasa
kampuni hiyo ina ndege tano zenye uwezo wa kubeba abiria sabini aina ya ATR
72-500, na ATR 42 yenye uwezo wa kubeba abiria arobaini na nane na ndege
nyingine tatu aina ya Boeng 737. Na sasa iko katika mpango wa kuongeza ndege
nyingine aina ya E- jets na ATR.
Mwisho … ///
No comments:
Post a Comment