22.11.13

Thursday, August 30, 2012

Wateja wa Presion Air kukata tiketi za usafiri kupitia huduma ya M-Pesa.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha kampuni ya Precision Air, Patrick Ndekana(kushoto)akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkataba na Vodacom Tanzania ambapo wateja wataweza kulipia tiketi za usafiri kupitia huduma ya M-Pesa,kulia ni Mkuu wa kitengo cha huduma za fedha wa Vodacom Tanzania Bw. Innocent Ephraim.

Mkuu wa kitengo cha huduma za fedha wa Vodacom Tanzania Bw. Innocent Ephraim,akionesha bango lenye maelekezo muhimu ya kufuatwa ambayo yatawafanya wateja wapate huduma ya kulipia tiketi za usafiri kupitia huduma ya M-Pesa kwa urahisi zaidi,kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha Precision Air, Patrick Ndekana.

Baadhi ya wafanyakazi wa Precision Air wakifatilia kiumakini mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na mkataba wa Vodacom Tanzania na kampuni yao ambapo wateja wa Precision Air wataweza kulipia tiketi za usafiri kupitia huduma ya M-Pesa

No comments: