Baadhi ya
watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini Mtwara,wakiwa katika hafla fupi
ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyoandaliwa na Vodacom
Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share.
Mkuu
wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami akimkabidhi mfuko wenye unga
wa kupikia ugali Bi.Chiku Mohamed aliepokea kwa niaba ya watoto yatima wa mkoa
huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia
kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom
Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia
kutoka kushoto ni Shekh Mkuu wa Mkoa huo Nurdin Mangochi Mkuu wa Vodacom kanda
ya kusini Bw.Mac Minja,Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji Bw.Hassan Saleh na
Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
Mkuu wa
Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami. akimkabidhi mfuko wenye unga wa
kupikia ugali Bi.Chiku Mohamed aliepokea kwa niaba ya watoto yatima wa mkoa huo
wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni
ya Ramadhan Care & Share inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa
mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia wapili toka kushoto ni
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Bw.Hassan Saleh, Mkuu wa Vodacom
Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
Mkuu wa
Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami,akimkabidhi mtoto yatima ndoo ya
mafuta ya kula Bi.Halima Juma, aliepokea kwa niaba ya watoto yatima wa mkoa huo
wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni
ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom
Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia
kutoka kushoto ni Shekh Mkuu wa Mkoa huo….Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini
Bw.Mac Minja,Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji Bw.Hassan Saleh na Mkuu wa
Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
Mkuu wa
Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw Ponsiano Nyami,wapili toka kushoto pamoja na
Shekh Mkuu wa Mkoa huo Bw.Nurdin Mangochi wakishuhudia Ofisa Mkuu wa Mauzo na
Usambazaji Bw.Hassan Saleh akimkabidhi ndoo ya mafuta ya kula mtoto yatima
Bi.Mwajuma Khamis aliepokea kwa niaba ya watoto wenzake yatima wa mkoa huo
wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni
ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom
Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mkuu wa
kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimhudumia mtoto
yatima Bi.Salha Haji uji mkoani Mtwara,aliefika kwenye hafla fupi ya
kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care &
Share inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi
Mtukufu wa Ramadhan.
Baadhi ya
watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Mtwara,wakifuturu wakati wa hafla
fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyoandaliwa na
Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care &
Share mjini humo.
Vodacom
yasaidia watoto yatima Mkoani Mtwara.
·
Ni kupitia kampeni ya Ramadhan Care and Share.
·
Ni katika mpango wa kuwathamini na kuwatambua
Watoto waishio katika mazingira magumu.
·
Kampeni ya Mtwara ni ya pili baada ya
kuzinduliwa mkoani Tanga.
Mtwara,Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki imetoa misaada mbalimbali
na kuwafuturisha watoto yatima na wa madrasa wapatao 500 mkoani Mtwara kupitia
kampeni yake ya Ramadhan Care and Share iliyo chini ya mfuko wa kusaidia
jamii”Vodacom Foundation”.
Misaada iliyotolewa kwa watoto hao ni pamoja na
vifaa vya kujifunzia, vyakula,mafuta ya kula, mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya Eid
el fitr ikiwa ni katika kutimiza malengo ya mpango huo uliozinduliwa mapema
wiki iliyopita mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa Ofisa Mkuu wa mauzo na usambazaji wa
Vodacom Tanzania Bw.Hassan Saleh, mwezi mtukufu wa Ramadhan ni muhimu kwa
waislamu wote nchini, sio tu kwa kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu, bali pia
ni kipindi kinachowapa nafasi ya kuwafikiria na kuwajali wale wasio na uwezo
ndani ya jamii yetu.
“Kwa miaka
mingi sasa, tumekuwa tunaendesha kampeni hii
katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunatambua kuwa Waislamu walio
wengi ni wateja wetu hivyo tumeona ni vyema kuwaenzi kwa kutoa kile
tulichonacho katika sehemu ya mapato yetu ili nao wajisikie kuwa miongoni mwa
jamii ya Watanzania,” alisema Saleh.
Kampeni ya Ramadhan Care and Share imekuwa njia
pekee ambayo Vodacom Foundation imekuwa ikiitumia
katika kushughulikia maswala mbalimbali yanayowakumba watoto yatima
waishio katika mazingira magumu. Kupitia kampeni hii maisha ya makundi
mbalimbali ya watoto yameweza kuboreshwa na kunufaika kutoka kwetu.
Kampeni hii ni moja kati ya kampeni nyingi ambazo
yetu imeanzisha katika kipindi cha Ramadhan. Tangu kuanza kwa Mwezi mtukufu
wateja wa malipo ya kabla wamewezeshwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa
maneno na kutumia intanet bila kikomo kwa shilingi 250 kwa siku.
Mwisho
No comments:
Post a Comment