KAMPUNI I-View Studios ya mjini Dar es Salaam
imeshinda mchakato wa kurekodi video mpya ya msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’
ambayo usaili wake utafanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, Dar es
Salaam.
Akizungumza mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema I-View imepata nafasi
hiyo kutokana na kiwango kikubwa cha video kadhaa ilizofanya lakini pia vifaa
ilivyo navyo na uwezo wa wafanyakazi wake.
“Siku zote kila mtu anaangalia kitu kizuri,
Diamond ametaka kufanya mapinduzi katika tasnia ya muziki, lakini kufanya
mapinduzi kunahusisha vitu vingi, tungo zake yeye kama msanii, studio
anayorekodia watu watakaoshiriki kwenye video yake kampuni itakayorekodi video
pia, lakini mwisho wa siku I-View chini ya Raqey Mohamed ndio imeshinda nafasi
hiyo.
“Raqey anafahamika kwa kazi zake pamoja na
kurekodi matangazo mbalimbali ya Televisheni, picha mnato lakini pia video za
wasanii Taznim ya Kwasakwasa, Utanikumbuka ya Suma Lee ni baadhi ya kazi ambazo
zinaonyesha uwezo alionao lakini pia Diamond na timu yake tumeweza kuona vifaa
vipya na vya kisasa ambavyo Raqey anavyo kwa sasa na hakuna kwa Afrika
Mashariki na Kati,” alisema.
Kwa upande wake Raqey ambaye ni Mkurugenzi wa
I-View alisema anahitaji kuifanya kazi hiyo kuwa tofauti ili kusukuma mbele
sekta ya mawasiliano na muziki kwa ujumla.
“Sisi kama I-View tunafurahi kufanya kazi na
Diamond, ni msanii mzuri na mkubwa ambaye kazi zake zinaonekana, hatutamuangusha
na mashabiki na wasanii wengine wasubirie kazi itakapotoka,” alisema.
I-View pia watashiriki katika mchakato wa kupata
watu watakaonekana kwenye video hiyo ambayo ni kwa mara ya kwanza nchini
kutafanywa usaili wa washiriki. Usaili huo utafanyika Jumamosi katika ukumbi wa
Nyumbani Lounge ambao unamilikiwa na mwanamuziki Lady Jaydee. Majina ya majaji
wataochuja yatanatarajiwa kutangazwa leo.
No comments:
Post a Comment