22.11.13

Thursday, September 13, 2012

TASWIRA YA DJCHOKA: Mwananyamala, Dar es Salaam

Kama dakika 15 zilizopita nilikuwa barabara ya Mwananyamala nikielekea Sokoni kuangalia vitu vya kununua ili kuweka nyumbani na maisha yaendelee. Pichani hapo juu ni maeneo ya kona ya Mwananyamala kama unatokea Kinondoni na kuelekea Mwananyamala Hosp, hii kuna kila siku kunakuwaga na foleni na hii inatokana na Daladala kubwa zinazosimama hapo kuchukua abiria na kuweka foleni kwa magari yanayotaka kukunja kona.

Kwenye soko la Mwananyamala nyanya fungu linauzwa kwa sh 300 hadi 400 so niliondoka na fungu zangu za 400 zakutosha kwa wiki kadhaa

Bei ya mchele kama unavyoziona zinaanzia shillingi 1700 hadi 2000 kwa kilo moja

Wakati narudi home nikapita njia hii ya Mwananyama kuja kutokea Kijitonyama so mvua ilikuwa ikinyesha mdogo mdogo na kifoleni jioni hii maeneo haya lazima tumeshazoea sisi wakazi wa huku

No comments: