NI MIAKA 10 SASA TANGU NIONDOKEWE NA
BABA MZAZI!!! WAS 'N FORM TWO NAKUMBUKA!! TAREHE KAMA YA
LEO "12th SEPTEMBER ALHAMISI"!!(KAMA UNANISIKIA BABA)
NI MUDA
MREFU SASA UMEPITA DADII... YAMEHAPEN MENGI HUKU NYUMA, SINCE
UTUACHE!! NILIMALIZA VIZURI O LEVEL, NA NIKAFAULU KWENDA
ADVANCE(A LEVEL) AZ U WISHED!!! SASA HIVI NIMEKUWA NA
NIMEMALIZA
CHUO MWAKA JANA...ZOO
ELIMU HAINA MWISHO SO NITAENDELEA NA KUSOMA!!! DADII
UNAKUMBUKA ULINIPIGA SANA KIPINDI NILIPOKUWA NAFUTA TAPES
ZAKO(CASSETS kanda) ULIZOKUWA UNANUNUA UKITOKA KAZINI, ZA WAKINA
AURLUS MABELE, PEPE KALE, DEFAO, NIMON TOKILALA NA AWILO
LONGOMBA!!
NILIKUWA NAZIFUTA NA KUJIREKODI MIMI NIKI
RAP!!!ILIKUWA MIAKA YA 90's NIKIWA PRIMARY, KIPINDI HICHO
BOLINGO NDIO IMETEK OVA BONGO... HAHAHAHA NIMEGUNDUA LEO
KUMBE NILIKUWA NAUFUTA UBOLINGO NA KUULETA UHIP
HOP!!NILIVUMILIA VILE VIPIGO VYAKO AND FINALLY A MADE IT
DADII...LEO NIMEKUWA MIONGONI MWA WASANII WAKUBWA WA MZIKI
HUU HAPA NCHINI!! NAAMINI WALA HAUKUWA UKILIOTA HILI KAMA
LITAKUJA KUTOKEA, MAANA KTK UKOO WE2 HAKUKUWA NA MTU
ALIYEWAHI KUFANYA MUZIKI, SEMBUSE HATA KUPIGA FILIMBI AU
MALIMBA....hahahahaha!! BUT NOW NIMEWAKILISHA VEMA FAMILIA, KITAA,
MKOA WA TANGA HADI SASA NGAZI YA TAIFA, LAKINI BABA
HAUPO NA WALA HAUYAONI HAYA MAFANIKIO...OOOHH DADII!!! A
WISH UNGEKWEPO...TUCELEBRATE ANA KU MISS MKE WAKO!!! ILA DADII
USIHOFU MAMA ANATUTUNZA VIZURI SANA, HADI TUMEKUA AISEE!!
RASHEED...OMAR...MAIMUNA...ASH A
WOTE TUKO POA BABA...NILICHUKUA HERUFI ZAO ZA MWANZO
NIKAZIUNGA NA NIKAIPATA R.O.M.A!!! NA SASA WATU WANANIITA
HIVO!!! DADII KITAANI UNAKUMBUKA WALIKUWA WANAKUITA DON KING??
KUTOKANA NA AFRO LAKO LA MVI KICHWANI...hahahaha STILL
WANANITANIAGA HIVO... DON KING SON!!! KILA NIKIKUKUMBUKA HUWA
NAJIFUNGIA ROOM NALIA SANA, KISHA NASALI NA MAISHA
YANAENDELEA...
LEO TUNAKUKUMBUKA NA TUNAADHIMISHA KUMBUKUMBU
HII WEEKEND HII IJUMAA HADI JUMAPILI, HUKO SAME MOSHI,
KWENYE NYUMBA YAKO YA MILELE!!
TUNAJIANDAA KWA SAFARI YA KUELEKEA HUKO, KUZURU KABURI LAKO!! NINA MENGI YA KUKWAMBIA ILA SIKU NIKIKUONA NITAKWAMBIA!!!
ULALE PEMA PEPONI BABA YANGU
MUSSA .A. MSHANA
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA
NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE
APUMZIKE KWA AMANI!!!
INNALILAH WAIN ALILAH RAAJIUN
AMEEN
TUNAJIANDAA KWA SAFARI YA KUELEKEA HUKO, KUZURU KABURI LAKO!! NINA MENGI YA KUKWAMBIA ILA SIKU NIKIKUONA NITAKWAMBIA!!!
ULALE PEMA PEPONI BABA YANGU
MUSSA .A. MSHANA
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA
NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE
APUMZIKE KWA AMANI!!!
INNALILAH WAIN ALILAH RAAJIUN
AMEEN
No comments:
Post a Comment