habari mabibi na mabwana!! poleni na mihangaiko ya siku!! naam
ijumaa iliyopita nilitoa
kibao changu maridhawa
kipya kabisa kinaitwa
2030!!!
na nilikiachia kwa
radio stations zote nchini
kadri ya uwezo wangu/wetu, though kutokana na
mawasiliano ni ngumu kufikia radio
zote kwa wakati, ila nyingi
ziliupata!!!
lakini niliweka
utaratibu fulani kwa watakaohitaji kuupata
huo wimbo 2030 mbali na radio basi wataupata kwa
kussuport kuununua on line
kwa tsh 3000/=!!nilishatangaza
sana mnafahamu!!ilikuwa ni trial
ya kuona nani ana love ya kussuport na nani hana kupitia njia zilizowekwa na sio njia nyingine.
zoezi limeenda
kwa challenge nyingi sana asante
wote waliossuport katika
hili, pia asante
kwa wale walioliharibu zoezi hili
maana imenifanya nimtambue
hu z real na hu z fake!!!
imeniuma kuona wapo wasanii wanafanya biashara
kama hii wanauza mix tapes, album,tisherts zikiwa
zote ni movements za kuleta
changes ktk mziki wetu, then hao
hao wanakuwa mstari wa mbele kupinga hii movement yangu halafu bila sababu yani dah SHALL WE MAKE
IT?????
nway lilikuwa ni zoezi
lililopangwa kufanyika kwa week
moja 1 tu ili kuona na kufanya tathmini
kuwa yanawezekana haya?najua wengi wanasubiri feed back ya mauzo haya
haikuwa nzuri sana kwa wingi wa nyomi nililokuwa nalo, lakini
pia haikuwa mbaya maana
ni mageni haya..kwa siku 7 za mauzo
ilikuwa kila siku wananunua watu
wasiopungua 50!! so unaweza
ona hapo kuwa
yanawezekana haya tukiyawekea
mkazo...ILA SIAMINI KAMA KILA MSANII ANAWEZA FANYA, INATEGEMEA NA NGUVU YA MSANII HUSIKA NA KIBAO
ALICHOKITOA..(IFIKIE KIPINDI
TUONGEE UKWELI TUU!!)wengi wameanza kufanya biashara kupitia
nyimbo hii na inawanufaisha wao,
wengi wamerecord radio wimbo huu kitu kilichopelekea kukosa quality na bado wanauzia wengine so wanapewa kitu kisicho na quality,
pia wengi wanakwazika na mengi yaliyoongelewa ndani ya wimbo huu na
wanakosa majibu maana wanakosa fursa ya
kuusikia mara kwa mara kwasababu hawajaunga mkono hii
movement!! au pengine imekuwa ni
njia ngumu kwao kuupata,
basi kwa wale
waliossuport kwa kuinunua nawashukuru sana na mungu awaongezee mlipopungukiwa,
najua litatokea hili la kujiona
wanyonge kuwa ROMA amechukua fedha
zetu na kisha ameachia bure, mi naamini ukiwa muelewa na ukiona
nilichokisema hapo juu hautakwazika as
long umeonyesha lav yako kwa
msanii unayemfeel, samahani sana kama nitakuwa
nimekukosea,nimefanya hivi kama
kuanzisha hiki kitu na naamini
wengine watafatia na
kukiboresha zaidi!!LAZIMA APOTEE
MMOJA ILI KUMI WAISHI VEMA NDIPO YATAPATIKANA MAENDELEO!! AM SO SORRY!!!
So leo wiki imetimia
na wimbo umetoka rasmi na hauuzwi tena
kama ilivyotangazwa awali.
unapatikana bure kwenye
net, download via access yoyote utakayoiona!! nimeutoa rasmi
kwenye blogs mbali mbali
ANZIA NA YA DJ CHOKA, na nyinginezo!!
Na version
iliyopita kuchezwa radio
ni version ya
ROMA ile beat yake iliyochangamka ambayo ni version ya 1 ambayo
ndiyo ilikuwa ya kwanza kutambulishwa ijumaa pale clouds fm radio.
kwa maswali zaidi
tutameet kwenye mainterviewz
huko maradioni na tutawekana sawa!!
samahanini kwa wote
niliowakwaza, asanteni kwa wote
mliossuport!!
13 comments:
kinyesi kizuri babu, huu ndo wakati wa kuelezana manake watoto wetu kweli hawatakuta hata makombo kamanda. Nice job.
Nigga Roma needs to work on his flow paterns,ujumbe mzuri lakini tunaishia kusikia kelele zakee na same flow bila vionjo...step up nicca!..CHOKA FIKISHA HUU UJUMBE
Good music and good Idea mi nimeipenda kaza mwend R.O.M.A kama watu wamezungumza mambo ambayo si mazuri na wengine kufanya biasharabila idhini yako nawaambia wote waliofanya hivyo huu si uzalendo hebu tuwe wazalendo halafu tuone itakuwaje......ni hayo tu piga kazi Mpaka kieleweke
NDO MAANA BAADHI YA WASANII HAWAENDELEI
KAMA NINYI KWA NYINYI
MNAKOSOANA
SISI TUTAFANYAJE!
DUH!
NGOJA NI DOWNLOAD NA MIMI
JAPO MCHAKATO ULIKUWA MZURI
ILA KWA MIMI
KUNUNUA SINGLE 1 KWA EF 3
LABDA MWAKA 2030
KAMA ULIVYOSEMA
Roma u r good bro... Anyone who dsnt respect aje kwngu nimpe darasa,,,, 2030 imetulia we need message not flow as long as ujumbe unafika..... Wanaheshimu Ramadhani wanazini mbele ya Shaaban hiiiiyyyyyooooo nimeipenda!!!
AMEBANA AMEACHIA!!!!!! HII NDO TANZANIA YEE MWENYEWE NDIE ALIEIMBA AFU AMEJISAHAU TENA,ALI2MIA AKILI KISODA SAHIZI NDO KAPEVUKA
dogo ametisha mbaya
HII NGOMA IKO POA ILA IMEKUWA REFU KM MWISHO IMEPOTEZA LADHA HIVI,ILA NA HUYO MTOTO KAIPENDEZESHA, WELL DONE ROMA.
..ROMA una ujumbe mwingi wa kutosha ila dizaini kama huimbi...unakuwa kama unasema/unahutubia vile, kumbuka kuwa na tight flow....kama unahutubia bana halafu mwishoni unakuwa kama unaharakisha hv.
as an mcee you are dowin good but one thing to remind u is that '' you are shouting behind the mic, au kuna mtu huwa unagombana naye kabla ya kuingia booth? hata kelele za FL studio kwa CUEBASe 5 na ASIO hazipo hivyo, panga vocal na siyo kelele kwa patterns zako wabongo watakuchoka si muda coz hutakuwa na tofauti na akina Madee walioshout kisha wakaishia! nataka mziki wako usichuje kama Afande, Fid na wengine kibao wa Hip Hop hapa Bongo, na ukiona vipi we kuja tu hapa mbagalani ntakupa jinsi ya kufanya na hits kibao tu toka my studio
ROMA ACHA NISEME HILI, MSG YA WIMBO NI TIGHT SANA ILA KWA NINI FLOW ZINAKUA ZILEZILE KILA NGOMA WE MJAMAA?! BADILIKA BANA TUTAKUCHOKA PIA HATA BEAT ZOTE MBILI ILE YA MWANZO NA HII YA PILI ZOTE ZIMEPOOZA SANAA! HAZIENDANI NA SPEED YA FLOW KAMA ILE YA MATHEMATICS, BADILIKA MZEE! AM OUT!
Nakubali kazi yako ni bonge la nyimbo lenye ujumbe mkubwa kwa jamii Roma mkatoliki unajua Mziki
ujumbe mzuri sema 2 hiyo stayl ya ku flow 2shaizoea..2badlishie stayl nyingine
Post a Comment