Nafikiria
kuanzisha msukumo wa kuleta curriculum mpya katika mfumo wa elimu wa
Tanzania ambayo inalenga matatizo yanayoikabili Tanzania. Curriculum
hiyo iwe ya kufundisha wanafunzi matatizo ya Tanzania na kujaribu
kuyapatia ufumbuzi. Namna hiyo wanafunzi watajiona kuwa wamewezeshwa
katika kubadili hali yao ya baadaye na mwelekeo wa taifa lao. Kwa hivi
sasa hali ya baadaye ya wanafunzi, watu na Taifa lenyewe iko katika
mikono ya
serikali tu. Kama wanafunzi wote, ambao ni kundi kubwa Tanzania,
watajifunza kuhusu matatizo yanayokabili taifa watataka kuchangia katika
mabadiliko kwa sababu maisha yao ya baadaye yanategemea hali hiyo ya
baadaye kwa taifa. Tunalenga wanafunzi kwa sababu ni kundi kubwa na wako
tayari kujifunza mambo mapya. Toa mchango wako hapa, tushirikiane
mawazo. Karibuni - Mr.Tz
Tunachojaribu
kufanya ni kubadili mwelekeo wa elimu Tanzania. Tutengeneza curriculum
ambayo inasaidia vijana kuwa na "critical thinking" Hii itawezesha
vijana hata wakiwa bado shule wanaanza kufanya projects za kutafuta
ufumbuzi wa maswala na matatizo yanayokabili taifa. Lakini yote
inahitaji nguvu ya serikali kuwa na waalimu hodari, vifaa mashuleni na
mambo mengine yanayomwezesha
mwanafunzi kujifunza.
Msanii wa kizazi kipya Mr.Tz anasema: "Nobody
can re-build Tanzania, other than us, the people of Tanzania.
Msifungamane na upande wowote. Tukiwa pamoja as the people of Tanzania,
we can, we WILL change Tanzania., for the better. Nisikilize.." - Mr.Tz
No comments:
Post a Comment