22.11.13

Friday, March 29, 2013

PROF JIIZE CLASSIC BARBER SHOP

 Hii ndio sehemu mpya aliyoifungua msanii mkongwe wa Bongo Fleva bwana Joseph Haule aka PROF JAY na ikapewa jina la PROF JIIZE CLASSIC BARBER SHOP. Barber Shop hii iko maeneo ya Msasani mwisho zamani palikuwa pakiitwa Chube.  Wafanya kazi wake ni makini kabisa na wazoefu wa kazi hizi za BarberShop.


 Kijana machachari kabisa wanamwitaga pacha wa Kanumba, ukifika hapo utakutana nae na atakutengeza vizuri kabisa kichwa chako na anauzoefu kwenye hii kazi na nimbunifu wa style mbalimbali za kunyoa nywele.

 TV kubwaaaaaa kabisa ikiwa full DStv iko ndani, kwa wale wapenzi wa mpira basi ukimaliza kunyoa kama hivi unaendelea kucheki mpira safii kabisa huku ukipata kipupwe murua na umeme ukikatika jenereta linawashwa fastaaaaaaaaaa

Ukinyoa ukapungukiwa na salio basi usikimbie wakala wote wapo wanapatikana hapo. 

 Pia huduma hizi zinapatikana

MTEJA KWETU NI NDUGU YETU

No comments: