22.11.13

Tuesday, April 30, 2013

(News) ALICHOKISEMA SHABAHA KUHUSU TUZO ZA KILI NA WACHAGUZI WA NOMINIES

Aliyekuwa meneja wa msanii sheta kabla ya kujitowa katika kundi la Dar Stahmina  anayejulikana kwa jina la Shabaha amefunguka na kuzungumza na HYPER HK kuhusu Malalamiko yako  juu ya mtu mwenye jukumu la kuwachagua watu wakwenda kuchagua washiriki wa TUZO za KILI MUSIC AWARD akiongea na mwandishi wetu alisema anaona asilimia kubwa wanaokwenda kwenye hizo academi zao ni watangazaji na wauza sura mjini hapa ambao wengi wao wanawasanii wao na mara zote kwenye hizo tuzo uvutia kwao ndio mana kila mwaka hakukosi malalamiko kwenye hizo TUZO. 

Aliendelea kusema kuwa yeye akiwa kama mtunzi wa nyimbo ambazo zilihit na kufanya vizuri ikiwemo NIMECHOKWA BWEGE MTOZENI na MDANANDA Pia ni msimamizi wa kazi za wasanii mbalimbali kwa muda mrefu sana katika game hii ya muziki wa bongo fleva. swali lake linakwenda moja kwa moja kwenye uongozi wa KILI MUSIC AWARDS kwamba wale watu wanaopangwa kuja kuchagua nominies wana sifa gani?  na je niwafatiliaji wa muziki na wanaujua muziki vizuri na nyimbo zilizokubalika kweli kwenye jamii?au kwavile ana jina tu la utangazaji apewe nafasi hiyo? na ni nani anaowachagua hao watu wanawachagua nominies?

No comments: