22.11.13

Sunday, May 26, 2013

(Audio) YABISI RECORDS na Ujio mpya wa MTC

Anakuja MTC,na ngoma mpya kwa jina "Hapa Hafungwi Mtu" inayozungumzia zaidi mateso na athari wanazopata washtakiwa wa kesi za kusingiziwa ikiwemo dhuluma,kupoteza mali, kufungwa kwa tuhuma ambazo hawakuhusika. Ikiwa ni real life experience,MTC anatarajia kuja na Album kamili January 2014. Hapa hafungwi mtu imerekodiwa katika studio za Noizmekah na ni single ya utambulisho na ujio mpya wa MTC anayemiliki Studio ya YABISI RECORDS, "Uwongo umejitenga kwenye Ukweli na sasa Yabisi Society itakuwepo tena Mtaani kama zamani,Hakipotei kitu" asema MTC..Pata kusikiliza ngoma HAPA na kwa mawasiliano zaidi check na +255 757 160 464 au +255 763 282 697 Support Tanzanian Hiphop

No comments: